We have 433 guests and no members online

KAMANDA SAIMON SIRRO: VITENDO VYA UBAKAJI NA ULAWITI VYAONGEZEKA JIJINI DAR ES SALAAM

1

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro amesema matukio ya Ubakaji na Ulawiti yameongezeka kwa kiwango kikubwa katika mwaka wa 2016 ukilinganisha na mwaka 2015 kutokana na matukio yaliyolipotiwa kiwa kipindi cha mwaka mzima.

Amesema hii inatokana na kuanzishwa kwa Dawati la Jinsia na pia wananchi kupata uelewa na kuripoti matukio hayo kila yanapotokea hii ndiyo sababu kubwa inayofanya kuongezeka kwa matukio hayo katika mkoa wa Dar es salaam.

Kamishna Saimon Sirro akizungumza katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati jijini Dar es salaam ametoa  taarifa hiyo wakati  akielezea takwimu za matukio mbalimbali yaliyotokea kwa mwaka 2016,

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro amesema  mwaka 2015 vitendo vya ubakaji vilivyoripotiwa vilikuwa 972 wakati mwaka  2016 vitendo vya kubaka vilivyoripotiwa vilikuwa 1030 ambapo ongezeko lilikuwa ni asilimia 58 ukilinganisha na matukio hayo kwa mwaka 2015.

Akitoa takwimu za vitendo vya kulawiti kwa mwaka 2015 amesema vitendo vya ulawiti vilivyoripotiwa ni 3010 ambapo  mwaka 2016 vitendo hivyo viliripotiwa kwa matukio 383 sawa na asilimia 73.

Amewataka wananchi kuacha matendo maovu kwani hayatawafikisha popote zaidi ya kuishia katika mikono ya sheria na kutupwa jela.

2

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro aksisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam.

4

Diana Masala Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akizungumzia msako uliofanywa kati ya Mamlaka hiyo na Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama ambapo ulifanikisha kukamata bidhaa mbalimbali za magendo.

5

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akiangalia silaha mbalimbali zilizokamatwa katika misako mbalimbali ya pilisi mwaka 2016.

6

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akieleza jambo kwa wanahabari wakati alipokuwa akionyesha silaha hizo.(P.T)

7

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro mitungi ya Shisha iliyokamatwa katika misako hiyo.

8

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja ya silaha ya kivita zilizokamatwa katika misako hiyo.

9

Baadhi ya maofisa mbalimbali wa polisi wakiwa wametandaza silaha hizo zilizoonyeshwa mbele ya waandishi wa habari.

10

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja ya bidhaa zilizokamatwa kwa pamoja na jeshi la polisi likishirikiana na Mamlaka ya Mapato TRA kulia ni Diana Masala Kaimu Mkurugenzi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

12

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha moja akionyesha moja ya mirija maalum inayotumika kutengenezea pombe haramu ya Gongo.

13

14

Kamishna wa Kanda Maalum  ya Polisi mkoa wa Dar es salaam CP Saimon Sirro akionyesha viroba vya bangi iliyokamatwa katika misako hiyo.

15

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA