We have 477 guests and no members online

Mkataba wa kiitifaki kutiliwa saini

media

Wajumbe wa Baraza Kuu la Maskofu nchini DR Congo (Cenco), Desemba 21, 2016.

Mkataba wa mazungumzo ya kisiasa kati ya upinzani na serikali unatarajiwa kutiwa saini hivi leo Ijumaa Desemba 30 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maaskofu wa kanisa katoliki wamekuwa wanaongoza mazungumzo haya na siku ya Alhamisi jioni walikutana na rais Joseph Kabila kuwasilisha nakala ya mkataba huo, kabla ya kutiwa saini leo jijini Kinshasa.

Maaskofu hao wamesema hawataki tena kuwepo kwa mazungumzo mengine huku wakisisitiza kuwa mambo ambayo hayakukubaliwa, yatamalizwa leo.

Maaskofu hao pia tayari wamekutana na ujumbe wa muungano wa upinzani wa Rassemblement. Sanjari na hayo pande zote mbili zimeelezea kukubaliana kwa masuala muhimu.

Kuelekea kutiwa saini kwa mkataba huu, maswali yanayoulizwa ni ikiwa rais Kabila amekubali kuondolewa kwa Waziri Mkuu wa sasa na kukubali atakayeteuliwa na Etienne tshisekedi? Na je, nini hatma ya wafungwa wa kisiasa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga Moise Katumbi?RFI

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA