We have 308 guests and no members online

Taasisi ya wanaharakati ya Bibi. Siti bint Saad yakutana na wanahabari

duu

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar .

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanaharakati Bibi Siti bint Saad, Bi Nasra Moh’d Hilali amewataka wanawake kushikamana kwa pamoja kupinga udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto .

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake ndani ya Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema udhalilishaji wa kijinsia umekithiri katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar jambo ambalo linapelekea kudhoofisha maendeleo nchini hivyo amewashauri akinamama kupiga vita vitendo hivyo .

Katika kupambana na vitendo hivyo Bi Nasra ameitaka jamii kujenga mashirikiano ya pamoja katika mfumo mzima wa malezi ya watoto na kuona watoto ni wa jamii na sio ya wazazi wawili pekee.

“Tujiunge kwa pamoja tuseme hatutaki udhalilishaji na tusiiachie Serikali pekee kwani suala hilo ni kubwa na linaathiri watu wengi kisaikolojia,”alisema Bi. Nasra

Alieleza tukio la hivi karibuni la mwanamke kuchomwa moto na mpenzi wake katika kijiji cha Paje linaonyesha udhalilishaji uliokithiri katika jamii na kuchangia kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Alifafanua kuwa kauli mbaya wanazotoa wanaume kwa wake zao zinachangia udhalilishaji uliowazi na amewataka akinababa kuwa na kauli nzuri kwa familia zao.

Aidha aliwataka akinamama kuwa tayari kutoa taarifa wanapobaini dalili za mtoto wa jirani anataka kudhalilishwa ili hatua za kuzuia vitendo hivyo ziweze kuchukuliwa kwa haraka.(P.T)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA