We have 241 guests and no members online

Barack Obama kuifunga Guantanamo Bay

Marekani

Barack Obama, rais anayeondoka madarakani Marekani

Taarifa kutoka katika Ikulu ya Marekani zinaeleza kuwa , inaonekana kwamba wafungwa zaidi kutoka katika gereza la Guantanamo Bay walioko kizuizini wanatarajiwa kuachiliwa kabla rais Barack Obama hajaondoka rasmi madarakani mpaka kufikia tarehe ishirini ya mwezi huu.

Rais Obama amesema kuifunga kambi hiyo ndiyo kipaumbele chake miaka nane iliyopita wakati alipokuwa akiingia madarakani, akitilia mkazo maelezo hayo ameongeza kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa gereza hilo kuna shusha hadhi ya wamarekani.

Akiieleze kambi hiyo amesema kwamba imekuwa eneo la mashaka, kushikiliwa kwa muda mrefu, kulazimishwa kula chini ya ulinzi , kunyimwa usingizi, nafasi ya dhiki, vipigo visivyokwisha , na aina nyingine ya mateso tele.

Hata hivyo idadi ya wafungwa imekuwa ikipungua kila uchao, na mpango wa kuifunga kambi hiyo ya mateso umekuwa ukipingwa na bunge la Congress.

Naye rais mteule wa Marekani Donald Trump, ametanabahisha dhahiri msimamo wake na kupinga wazo la kumuachilia mfungwa yeyote kutoka katika gereza hilo. Akiweka bayana msimamo huo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter amesema kwamba wafungwa hao ni watu hatari na hawana ruhusa ya kurejea katika uwanja wa vita.BBC

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA