We have 233 guests and no members online

Yahya Jammeh aungwa mkono na jeshi la Gambia

media

Rais aliyeshindwa uchaguzi wa urais nchini Gambia, Yahya Jammeh akataa kuondoka mamlakani..

Mkuu wa majeshi nchini Gambia ametangaza kumuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya Jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo, huku upinzani ukimtaka rais huyo kutothubutu kusalia madarakani ifikapo Januari 19.

Katika barua kwa magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litamtii rais huyo.

Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.

Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.
Hivi karibuni kambi ya Adama Barrow aliyetangazaw mshind wa uchaguzi wa urais, lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.

Hatua hiyo ya jeshi inaonekana kuzua hali ya sintofahamu katika kuanzisha serikali mpya baada ya Jammeh aliyekuwa madarakani kwa miaka 22.

Mapema mwezi Desemba 2016 Muungano wa wanasheria nchini Gambia ulisema kuwa kitendo cha rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kukataa matokeo ya kura zilizoonyesha kuwa ameshindwa katika uchaguzi uliopita ni kuisaliti nchi hiyo.

Hapo awali Jammeh alikubali kushindwa na kuahidi kuondoka madarakani lakini aliyakataa matokeo ya uchaguzi siku chache baadaye.RFI

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA