We have 316 guests and no members online

Babu Wa Old Trafford Na ' Ushamba' Wa David Beckham!

Image may contain: 1 person

Ndugu zangu, 

Kwenye kitabu chake, Babu wa Old Trafford, Sir Alex Fergussson anasimulia kile ambacho sasa kinatusaidia hata kujua ni kwanini ikatokea siku ile, Babu wa Old Trafford akapandwa hasira na kumrushia kiatu cha usoni David Beckham.

Babu wa Old Trafford alimuona Beckham aliyekuwa akibadilika tabia na kuwa kijana wa majigambo. Beckham amelelewa kwenye taasisi ya Man United, tangu utotoni.

Akiwa na miaka 16 tu nyota yake ikaanza kung'aa. Na ilipong'aa zaidi, Beckham akaanza kuota mapembe. Kila alipokwenda macho ya media, warembo na washabiki yalikuwa kwake. Beckham akamezwa na umaarufu. Akaanza tabia za ' Kishamba'. Na pesa zilipoanza kujaa kwenye akaunti, Beckham akaanza kuhangaika zaidi na vitu vya kuonekana, mavazi na magari. 

Babu wa Old  Trafford anasema, na ni ukweli, kuwa binadamu hangaika kwanza  na kinachokuletea heshima na kipato chako. Hivyo kazi yako. Kwa Babu wa Trafford, mpira ni kazi, na inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwa aliyeamua kuifanya kazi hiyo.  Babu anasema, nguo karibu kila mtu anavaa, gari nzuri zinaendeshwa na wengi hapa duniani. Wenye nyumba nzuri alikadhalika.  Hivyo, ' ushamba' ni binadamu kuhangaika na kujionyesha na nguo zake alizovaa, au gari yake anayoendesha.

Na mazoezini  Beckham akawa si yule wa zamani. Akafikia hata kumbishia Babu wa Old Trafford aliyemlea.

Beckham akawa anajali zaidi anavyoonekana ikiwamo kubadili mitindo ya nywele kuliko yenye kuhusiana na mpira.

Siku moja, katika ' Ushamba' wake, Beckham alidiriki kuingia na kofia hata mgahawani akiwa na wachezaji wenzake.

Uungwana na kwa maana hiyo, kuwa Gentleman ni pamoja na kuvua kofia unapoingia sebuleni au mgahawani.

Babu wa Old Trafford akamwambia Beckham avue kofia. Akakataa.

Kumbe, katika ushamba wake, Beckham alikuwa amenyoa staili mpya ya nywele na alitaka media ione jioni ambayo angecheza mechi!

Naam, kuna wasanii wa Bongo waliimba; "Ushamba ni mzigo!".

Maggid.

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA