We have 233 guests and no members online

NIMEKUMBUKA KAULI ZA JKN NA JFK

Picha ya Fred Matuja

Nianze makala hii fupi kwa kuwatakiwa Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2017. Nina imani kila mmoja ameweka malengo na mipango ya kumfanya aishi maisha yenye ufanisi kwa kuchangia kukua kwa uchumi wake binafsi ambao katika picha kubwa utakuwa na athari katika uchumi na maendeleo ya jamii inayokuzunguka na tuna tumai mguso huo utaligusa taifa letu zuri Tanzania. Tanzania ni nchi yetu, tunao wajibu wa kuipenda, kuilinda na kufanya kila liwezekanalo iwe mahali pazuri pa kuishi kwa maendeleo endelevu.

Najaribu kumbuka muasisi wa Taifa letu. Wakati wa uhai wake, baba wa Taifa la Tanzania na mmoja wa wapigiania uhuru wa nchi hii na Afrika kwa ujumla. Mwalimu Julias Nyerere, katika moja ya nukuu zake aliwahi kusema; kama kweli maendeleo yanafanyika, lazima watu wahusike( If real development is to take place, the people have to be involved.) kama ingekuwa lugha ya michezo, basi kila Mtanzania anatakuwa kuwa sehemu ya mchezo unaoitwa kujihusisha na maendeleo.

Kwa namna alivyozungumza Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake, kauli yake inashabihiana kabisa na kauli mbiu ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inayosema, “kwa pamoja tunalijenga Taifa”. 
Msingi wa kauli zote hizi kwa zina akisi msemo wa umoja ni nguvu. Na nguvu yetu ni umoja wetu katika kuijenga nyumba yetu inayoitwa Tanzania. Wakati wa ujenzi wa nyumba yetu Tanzania, kuna ulazima wa kuishi kwa mtazamo wa kipiganaji dhidi ya maadui wa nchi hii hasa umasikini, ujinga na maradhi. Kwa upande mwingine kuna maadui kama vile rushwa, ufisadi na ubinafsi wanaotengenezwa na maadui mama ambao ujinga na umasikini.
Na umasikini mbaya zaidi ni wa kifikra na ubinafsi unakuzwa na baadhi ya viongozi au watu wenye dhamana ya kuongoza kwa namna yoyote ile.

Ninapotaja kiongozi, sina maana ya kiongozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa pekee, bali kiongozi wa kiufundi (technical leader) kama vile waandishi wa habari, makala na wataalamu mbalimbali tulionao nchini humu wanaoweza kuwa sehemu ya suluhisho la matatizo yanayoendelea nchini kwetu.

Mtu mmoja aliwahi kusema, mtu yeyote maarufu au mkuu hufikia ukuu baada ya kutatua matatizo ya watu wake. Tanzania kuna matatizo na changamoto chungu mzima, kwa lugha nyingine, matatizo ya kijamii na changamoto hizi fursa kwetu sisi kuzitatua kwa kuonesha suluhisho ili jamii isogee mbele zaidi. 
Tanzania ikiendelea, kila mmoja atafaidi. Kwa pamoja tukiamua kwa dhati kucheza nafasi zetu ili Tanzania isonge mbele kimaendeleo, tutafanikiwa.

Nihitimishe kwa kumnukuu Rais wa 35 wa Marekani John Kennedy anaekumbukwa mpaka leo kwa kile alichowaambia watu wake mara baada ya kuchaguliwa mwaka 1960. Kennedy alimtaka kila mmoja ajiulize ataifanyia nini Marekani.

Taifa letu kwa sasa lina takribani watu milioni zaidi ya 50. Tukipata jitihada ya pamoja ya msukumo wa maendeleo walau kwa watu milioni 20 pekee watakofanya kwa nguvu, juhudi na maarifa ili tupige hatua, bila shaka Tanzania itakuwa kwa haraka kiuchumi na kuwa moja ya mataifa ya mfano wa kuingwa duniani.
Kwa pamoja tulijenge taifa letu.

Fredrick Matuja
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.(P.T)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA