We have 465 guests and no members online

WAZIRI MKUU AONGOZA MAMIA KUMZIKA KAPTENI MHAIKI

01

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na mkewe Mery Majaliwa wakiweka shada la maua katika kaburi la aliye kuwa Mkuu wa ndege za serikali Kapteni  Kenan Mhaiki  aliye fariki tarehe 31/12/2016 nakuzikwa tarehe 4/1/2017 kijijini kwao Matogoro Mkoani Ruvuma. Picha na Chris Mfinanga

02

Mke wa Marehemu  Kapteni Kenan Mhaiki  akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake.

03

Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Muahiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao.

04

05

Waziri mkuu Kassim Majaliwa  akitoa salamu za serikali katika misa ya kumuombea maerehemu Kapteni K enan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea  Parokia ya Mtoto Yesu  Matogoro Songea.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wakazi wa mji wa Songea na kata ya Matogoro kuuaga mwili wa aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki katika ibada iliyofanyika kwenye parokia ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu iliyoko Matogoro, mjini Songea.

Waziri Mkuu ambaye ameshiriki msiba huo kwa niaba ya Serikali, pia alishiriki mazishi ya Kapteni Mhaiki ambaye pia alikuwa rubani wa ndege za Serikali yaliyofanyika kwenye makaburi ya parokia ya Matogoro.

Akizungumza kwenye ibada ya mazishi mara baada ya kutoa heshima za mwisho, leo jioni (Jumatano, Januari 4, 2017), Waziri Mkuu aliwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

“Msiba huu ni wetu sote na umetugusa wote. Ni msiba mzito kwa wanafamilia na kwa Serikali pia. Kapteni Mhaiki amekuwa rubani wa ndege za Serikali kwa muda mrefu na amewaendesha viongozi wa kitaifa kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya tano. Kwa niaba ya Serikali tunawapa pole sana,” amesema.

“Ninawaomba wafiwa wote hasa mke wa marehemu na watoto tushikamane katika kipindi hiki na tuendelee kuwa wavumilivu huku tukimuombea Baba yetu apate pumziko la milele,” amesema.

Kapteni Mhaiki alifariki dunia Desemba 31, 2016 katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam. Alilazwa katika hospitali hiyo, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa ugonjwa wa saratani ya ini.

IMETOLEWA NA

OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMATANO, JANUARI 4, 2017.(P.T)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA