We have 261 guests and no members online

SERIKALI KUENDESHA MPANGO WA KUTATHMINI NA KURASIMISHA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO

Na Daudi Manongi-MAELEZO

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA wanaendesha mpango wa kutathmini na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo rasmi wa Mafunzo.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu wa Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Eric Shitindi, imesema kuwa mpango huo unatoa fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi, kupewa mafunzo, kuziba upungufu na kisha kutunukiwa cheti.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa sifa za mwombaji wa mafunzo hayo ni pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitano na umri usiozidi miaka 45.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa fani mbalimbali zitakazohusika ni Uashi, Useremala, Ufundi Magari (makenika), upishi, uhudumu wa hoteli, Bar na Migahawa.

Ili kufanya maombi waombaji wanatakiwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya  iliyoko karibu ili kuchukua fomu za kujaza maombi bila malipo yeyote na maombi hayo kuwasilishwa kuanzia tarehe 5 hadi 25 Januari 2017.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali na pia watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa ajili ya usaili kuanzia Tarehe 10 Februari 2017.

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA