We have 246 guests and no members online

Watanzania tutaendelea tukiamua na hatutaendelea tukiamua

Picha ya Fred Matuja

Mwanafalsafa wa Kigiriki, Aristotle aliwahi kusema sisi wanadamu tunakua jinsi tulivyo kutokana na mambo tunayorudia kuyafanya mara akwa mara. Hivyo basi, ubora katika mambo si kitendo bali ni tabia. (Excellence, then, is not an act, but a habit)

Kimsingi tabia zetu nikilenga Watanzania, zimeundwa au ni matokeo ya utamaduni wa kimaisha tunaokuwa nao kuanzia ngazi ya familia, jamii na hatimae Taifa zima. Mimi binafsi kama mtu niliepata kujifunza somo la saikolojia wakati nafanya mafunzo ya elimu (au ualimu kama inavyodhaniwa na wengi) nilipata fursa ya kujifunza mambo ya msingi kutoka kwa wataalamu wa tabia za binadamu. Kuna moja ya msemo wa watalamu hawa unasema; “panda mbegu vuna kitendo, panda vitendo vuna tabia, panda tabia vuna mwenendo, panda mwenendo vuna hatima ya mtu, jamii na taifa katika ujumla wake” 

Tabia zina nguvu sana katika maisha ya watu. Sababu hii inatokana na hali ya kujirudia kwa vitendo tunavyofanya wanadamu kila siku. Na kwa kuwa hali ya kujirudia inakua katika mifumo ya akili, kuna wakati matendo tunayafanya bila hata kufikiri.
Mfano, kwa dereva wa gari mwenye uzoefu wa muda mrefu, anaeweza kuendesha gari lenye “gear ya manual”, na kuna wakati hata akili haifiri kwanini uingize gia moja baada ya nyingine. Ndivyo ilivyo kwa jambo lolote ambalo mtu anafanya kila siku. 

Watanzania kama taifa kuna haja ya kijikagua na kujitathmini kwa namna tunavyofikiri na tunatoa wapi taarifa za kulisha akili zetu. Tabia zinapojionesha kutendeka katika maisha yetu hata bila kufikiri, kila siku, zinaonesha mwenendo wetu na tunaweza kupima ufanisi wa mtu au kinyume chake. 

Kama alivyosema Horace Mann, mmoja wa waelimishaji wakubwa duniani, aliwahi kusema, tabia ni kama nyaya za umeme. Tukiwekeza mifumo ya aina fulani ya kifikra na kitabia kama familia ambazo zikiungana huzaa jamii, tunaweza kupata matokeo tunayoyataka sawia na mbegu ambayo tumewekeza katika fikra zetu.

Ili kuwa na mtazamo wa pamoja, naomba kutoa tafsiri ya tabia kutoka chanzo kimoja. Tabia ni muunganiko wa maarifa, ujuzi na shauku au tamaa ya mtu. 

Nikikumbuka kile nilichojifunza chuo cha ualimu, msingi wa kupata au kujiongezea maarifa ni pale mu anapoingiza taarifa katika ufahamu wake ili kujielimisha kupitia mfumo rasmi wa elimu (formal education), mfumo rasmi wa elimu ili kukidhi malengo maalum (non-formal education) na elimu isiyo rasmi (informal education).

Kuna siku tunaweza kudadavua mfumo rasmi wa elimu na elimu rasmi yenye lengo maalum, ila kwa leo nataka nijikite kwenye elimu isiyo rasmi ambayo hupatikana kupitia vyanzo mbalimbali kama vyombo vya habari (mathalani majarida, magazeti, radio, TV na tovuti mbalimbali), mijadala vijiweni, mijadala kwenye makundi maalum kama mitandao ya kijamii (facebook, twitter, watsapp, viber n.k) vitabu kutoka kwa waandishi mbalimbali na vyanzo mbalimbali vinavyoweza kutoa “lishe” ya maarifa katika akili zetu. 

Katika eneo ambalo kama sisi kama taifa tuna haja ya kufanya tathmini ya mara kwa mara (normative evaluation) ni namna gani taarifa zilizo “vijiweni”, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna vinavyo athiri namna ya watu wanavyofikiri, hivyo kuzaa matendo yasiyotarajiwa, ambayo huzaa tabia hasi zinazojenga mwenendo hasi kuhusu mitazamo ya baadhi ya wananchi juu ya viongozi hususani nyakati hizi. 

Watanzania hatuna budi kuamua kwa pamoja ili kukiponya kizazi cha leo na kijacho ambacho kitachukua majukumu ya kulea familia zitakazokuwa sehemu ya jamii na taifa kwa ujumla.

Kuna mambo ambayo baadhi ya nchi zingine Afrika au bara la Asia wanafanya leo, sisi hatufanya kutokana na namna tunavyofikiri na kuamua kutenda kama mwitikio wa nini kipo katika fikra zetu. Hii yanikumbusha msemo wa Hery Ford bilionea mwanzilishi wa kumpuni ya magari ya Ford, alisema, tukifikiri tunaweza au hatuwezi sote tuko sawa. (If we think wa can or we can’t we are all right). Tuna wajibu wa kufkiri tunaweza kama wazalendo kwa ajili tu ya heshima ya utaifa wetu kwa kizazi kijacho. 

Natoa rai kwa serikali, taasisi za kidini, asasi za kiraia na vyama vya siasa; kuna haja ya kuanza kufikiri kwa pamoja kuhusu uzalendo na maslahi ya Taifa hili kwa nia njema ya pamoja bila kujali tofauti zetu za ki-itikadi, ki-imani hali kadhalika ki-ushabiki wa timu za michezo iwe ni mpira wa miguu, kikapu au pete.

Ukipata wasaa wa kuzungumza na wataalamu wa program za kompyuta hususani walio-bobea kwenye fani ya “programming”. Mfumo wa kutengeneza program unakusudia kutoa matokeo ya mtengeza program amekusudia kupata. Nadhani kuna watu kwa kukusudia kupitia elimu isiyo rasmi wanafanya programing ya akili za Watanzania hususan vijana, na katika hili si kwa lengo jema. Naomba kukukoselewa kama nakosea. Ila nadhani niko sahihi. 

Ili kulikoa taifa, moja ya njia ya mfumo usio rasmi wa elimu ni kuja na program tofauti ya kuwapa Watazania, hususani vijana taarifa mbadala ili kubadili namna ya kufikiri, ili kupata upya namna ya kutenda, kupanda tabia mpya, mwenendo mpya na hatima mpya kwa mtu mmoja mmoja, hatima mpya ya familia zetu na hatima ya taifa letu.

Uzalendo ni somo muafaka kwa ajili ya maslahi ya taifa kwa sasa. Liwe na mijadala vijiweni, kwa mitandao ya kijamii na kila eneo ambalo vijana wamewekeza akili zao huko. Taifa laTanzania ni lazima lisonge mbele. Ni shauku yangu kila mmoja acheze nafasi yake tuamue kwa pamoja kwenda mbele. Namna ya pekee kuanzia ni elimu ya uzalendo ambayo ina vyanzo vingi vya kuitiririsha kuwafikia Watanzania wengi kwa maslahi mapana ya nchi hii.

Mungu ibariki Tanzania. Kwa pamoja tuijenge nchi yetu!

Fredrick Matuja
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.(P.T)

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA