We have 467 guests and no members online

Simulizi Za Kusisimua: Vijana Wa TANU WENYE MSIMAMO MKALI WALIMPINDUA MWAPACHU MLIMANI

Image may contain: one or more people

Ndugu zangu, 

Mwanazuoni Born Again Pagan anaandika kutoa ufafanuzi wa kilichotokea Chuo Kikuu Mlimani enzi hizo na hata kupelekea kufanyika kwa mapinduzi yaliyoiondoa Serikali ya Wanafunzi iliyoongozwa na Juma Volter Mwapachu.

Born Again Pagan anaandika:

" Mwenyekiti,

Uliandika sehemu ya maelezo kutoka kitabu cha Rais Yoweri Museveni, Sowing the Mustard Seed, kuhusu msuguano uliojitokeza Museveni alipokuwa bado ni mwanafunzi hapo Mlimani na Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Msimamo Mkali (University Student African Revolutionary Front – USARF, kwa upande mmoja, na uongozi wa Chama cha TANU Youth League, Tawi la wanafunzi wa Mlimani, kwa upande wapili. Ni kweli msuguano huo ulijitokeza. Lakini hukueleza ulijitokeza mwaka gani na chini ya uongozi wa akina nani waliokuwa upande wa Chama cha TANU Youth League? Pengine, sikuisoma vizuri hiyo uliyoandika. Endapo hukufafanua, naomba kutoa maelezo ya kuondoa utata uliopo, kama ifuatavyo:

Wanafunzi Watanzania waliporudishwa kwenye vyuo vikuu vyao (baada ya msamaha wa mgomo wao wa Jumamosi, tarehe 22, Oktoba, 1966) walikuta mfumo wa serikali ya wanafuzi hao umebadilika au niseme serikali za wanafunzi wa vyuo vya juu zilipigwa marufuku. Badala yake walitakiwa maslahi yao yaongozwe na Chama cha Vijana wa TANU (TYL).
Hapo Mlimani, wanafunzi walikutana na kuchagua viongozi wao: Juma Volter Mwapachu alichaguliwa Mwenyekiti, Oliver Maruma, Katibu na Samwel Frederick Mwekahazina. Pamoja na kufungua tawi hilo, Makao Makuu ya Vijana na TANU yalipandisha Tawi la Mlimani kuwa na hadhi ya Tawi la Wilaya na kupewa gari la Volkswagen Combi kwa shughuli za Tawi; dereva wake alikuwa ni Samwel Frederick.
Nafikiri msuguano ulijitokeza wa uongozi wa Mwenyekiti Juma Mwapachu, ambao baadhi ya wanachmma wa TYL waliona ni wa kinafiki.
Karibu kila alhasiri ya Jumatano, wanafunzi walikuwa hawana masomo yaliyopangwa; walikuwa huru. Wanachama wa TYL walijiwekea utaratibu wa kujitolea kukusanya korosho zilokuwa zimeiva na kuanguka chini hapo Mlimani au kwenda Ubungo, Manzese na Magomeni kusaidia kufundisha kisomo cha manufaa (elimu ya watu wazima.)
Na viongozi wa TYL walikuwa wakichukua hiyo Combi kwenda makao makuu ya vijana kikazi. Lakini mara ikasemekana kuwa walikuwa wakienda kwa mambo yao binafsi jijini baada ya mikutano hiyo.
Kuna Jumamosi moja wana-TYL walienda kujitolea kusaidia wanakijiji kuvuna mpunga huko Bagamoyo. Combi liliwapeleka na kuwarudisha Mlimani. Lakini jioni hiyo hiyo, uongozi wa TYL ulichukua hilo Combi hadi Muhimbili kuwabeba baadhi ya wasichana waliokuwa wanachukua kozi ya unesi hadi Kambi ya Kujenga Taifa ya Ruvu kucheza dansi lililokuwa limetayarishwa na Mkuu wa Kambi, Afande Mushi, aliyekuwa rafiki ya uongozi huo wa TYL Mlimani.
Kutoshiriki kazi za kujitolea na matumizi mabaya ya Combi, kulichafua uhusiano baina ya uongozi na wanachama wa TYL wenye msimamo mkali, waliopanga namna ya kuweza kuutoa uongozi wa Juma Mwapachu. Mkutano uliitishwa siku moja jioni na kutoa malalamiko na kisha kupigakura ya kutounga mkono uongozi huo kwa kura za kishindo. Yakawa ni mapinduzi makubwa bila kumwaga damu. Viongozi wapya walichaguliwa: Mwenyekiti akawa Andrew Shija, Makamu wake Brendire Moronda, Katibu Ali Mchumo na Mwekahazina Charles Kileo. 

Ni kwanini basi, Museveni, Rais wa USARF alishiriki pia vikao vya ndani vya TANU YOUTH LEAGUE?

Itaendelea kesho..

BORN AGAIN PAGAN

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA