We have 232 guests and no members online

Rais wa zamani wa Ureno Mario Soares afariki dunia

media

Mario Soares katika studio za RFI, mwaka 2013.

Mario Soares ambaye anachukuliwa nchini Ureno kama Mwanademokrasia amefariki dunia Jumamosi hii Januari 7 akiwa na umri wa miaka 92, msemaji wa hospitali ya Lisbon ambapo alikuwa amelazwa amesema.

Mario Soares alilazwa hospitalini Desemba 13 akiwa katika hali mbaya. Afya yake ilidhoofika baada ya kifo cha mke wake mwezi Julai mwaka 2015. Baada ya ya matibabu ya muda mfupi, rais wa zamani wa Ureno alipoteza fahamu kwa muda mrefu toka Desemba 26, kufuatia " maradhi ambayo hayakuweza kutajwa.

"Mimi ni mtu wa kawaida"

Mwanzilishi wa chama cha Kisoshalisti nchini Ureno, Waziri wa Mambo ya nje, Waziri Mkuu mara mbili, rais kuanzia mwaka 1986 hadi 1996 na kisha Mbunge wa Ulaya, Mario Soares alikuwa kiongozi muhimu katika demokrasia ya Ureno.

"Mimi kamwe sijichukulii kama mtu wa ajabu. Mimi ni mtu wa kawaida," Mario Soares alisema katika mahojiano yaliyochapishwa mwezi Februari 2015. Mario Soares, mwanasheria aliye ingia katika siasa kama mpinzani katika utawala wa udikteta wa Antonio de Oliveira Salazar.

"Kuna watu ambao tayari wamesha endeleza na wataendeleza demokrasia yetu. Hatuna haja ya kuwa wale au kuwa katika chama kimoja na itikadi moja ili kutambua walichochangia kwa nchi hii, amesema rais Marcelo Rebelo Sousa, ambaye ni kutoka chama cha kihafidhina. "Kizazi changu kimeishi daima katika uhuru na uhuru huu tuliupata kupitia mikononi mwa Mario Soares", amesema Meya wa mji wa Lisbon, Fernando Medina ambaye ni kutoka chama cha Kisoshalisti.RFI

Tuma Maoni


Security code


Anzisha upya


Karibu Mjengwablog

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

We are Hiring - Senior Web / Mobile Deve…

As we are expanding our operations , W...

Soma zaidi

Job Vacancy: Business Administrative Ass…

The primary role of the business admin...

Soma zaidi

JOB: Sales and Marketing person for sell…

BANIZ SAFARI is one of the project ava...

Soma zaidi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...

Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...

Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

bshyera11_ba222.jpg

Smartads

 

Maoni ya Watembeleaji

BLOG SHABIHANA