michezo

Habari Za Uhamisho Na Fununu Zake: Juventus Wametoa Ofa ya EURO 60m Kwaajili Ya Kumnasa Morata.

on

Juventus wako tayari kuilipa timu ya Chelsea kitita cha EURO 60 million kwa ajiri ya mshambuliaji Alvaro Morata.

Tukumbuke kuwa mchezaji huyo wakiispania aliwahi ichezea timu hiyo mwaka 2014 hadi 2016, Kabla ya kurudi katika klabu yake ya Real Madrid na kuuzwa kwenda Chelsea msimu ulopita.

Baada ya kuwa na msimu mbovu ndani ya klabu hiyo ya Chelsea, Juventus wanaimani kumsajiri mchezaji huyo kwa mkopokwa kitita cha EURO 15m kujumlisha na makubaliano ya kumsajiri moja kwa moja kwa EURO 45m kurudi kuichezea tena klabu hiyo pale Turin.

 

 

Man Utd wamejiandikisha kumsajiri Kluivert.

Manchester United wanahamu ya kumsajiri mshambuliaji wa Ajax Justine Kluivert.

Justine mwenye umri wa miaka 18 amekuwa moto kwa Europe’s baada ya kufunga magori 29 kwa Ajax msimu huu.

Repoti zinasema kuwa Kluivert yuko tayari kubadilisha mkataba wake ili kumfanya kuwa mchezaji anaelipwa zaidi pale ajax kwaajiri ya kujaribu soko msimu wa majira ya joto.

 

Gerrard amekubaliana kufanya kazi kwa miaka mitatu katika klabu ya Rangers.

Steven Gerrard amekubali mkataba wa miaka mitatu kuifundisha klabu ya Rangers kama kocha mkuu.

Mchezaji huyo wa muda mrefu wa klabu ya Liverpool atatambulishwa rasmi Ibrox haraka kwaajiri ya kuanza kibarua chake cha kwanza kama kocha mkuu.

Gerrard atachukua nafasi ya Graeme Murty na kibarua chake kama kocha mkuu ndani ya Cetric nchini Scotland.

Na

-Innocent Chambi-

About Innocent Chambi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *