KwanzaJamii Tv

Halotel Z’bar yatoa msaada kwa waislam katika mfungo wa Ramadhan

on

Kampuni ya halotel imesema itahakikisha wanaifikia Misktiki ya Mjini na Vijijini visiwani hapa ili kutoa futari (Chakula) bure kwa waumini wa kiislam, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaendeleza ushirikiano wao na wananchi wa Zanzibar hadi katika mwezi huu mtukufu.

Mkuu Idara ya Biashara Zanzibar, Peter Mosha akizungumza baada ya kutoka msaada huo maeneo ya Kikwajuni Mjini Unguja, alisema hiyo ni moja ya mambo ya msingi kwa kampuni hiyo katika suhirikiano wao na wananchi.

“Kwa kuwa sisi ni sehemu ya jamii tumeona hakuna budi kushuka kwa wananchi wa chini ili kutoa msada wetu huu, ambao unalengo kusaidia katika kipindi hichi cha mwezi wa Ramadhan”alisema Mosha.

Mosha alisema hatua hiyo ya awali ambayo imeanza katika maeneo na Miskiti ya Mjini lakini pia wanatarajia kufika katika maeneo mengine mbali mbali ikiwamo ya vijijini ili nako waweze kutoa msaada wao kwa wananchi.

Alisema hawafanyi hivyo kama kujitangaza kibiashara bali wanafanya kwa moyo wao mwema wa kuisadia jamii ya kiislam ambayo imejitolea kufunga ndani ya mwezi huu.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo ofisi ya Zanzibar, Abdulla Iddi Abdulla alisema hatua hiyo ni moja ya kuwaunga mkono waislam visiwani humu wale wanaotumia mtandao wao na hata wasiotumia.

“Kwa kuwa huu ni mwezi mwema nasi tumeona ni bora kutenga fedha maalum za kusaidia chakula waislam katika kipindi chote cha mwezi hu, kwa kuanzia tumeanza katika Miskiti ya Mjini lakini baadaye tutafika hadi vijijini”alisema.

Naye  Sheikh Sheikh Omar Said alisema  hatua ya kampuni hiyo kutoa msaada wao huo ni ya kupongezwa na kuungwa mkono, huku akiwataka waislamu nchini kufuata mafundisho ya dini yao ili kujenga jamii yenye maadili na upendo miongoni mwa wananchi.

Aliwataka Waislam kuutumia mwezi huu wa ramadhani kuwa ni fursa kwao kwa kuzidisha ibada na kutenda wema kwa wananchi wengine, huku akisisitiza haja ya kutoa msaada kwa masikini kuwa ni kitu muhimu sana ili asiwepo muislam ambaye ameachwa nyuma.

Kwa upande wa baadhi ya waislam walionufaka na sadaka hiyo ya Futari walisema hatua ya kampuni hiyo ni ya kupongezwa na kuungwa mkono, kutokana na kujali maslahi ya wananchi hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan

Walishauri na kampuni nyengine pamoja na matajiri kutumia uwezo walionao kusaidia wananchi mjini na vijijini, wakiwa na lengo la kutekeleza wajibu wa kusaidia wanyonge kwa waliyonacho.

Mbali ya hatu hiyo kampuni hiyo pia imezindua huduma maalum ya inayojulikana kwa jina la “hodi Hodi’ huduma ambayo ni maalum kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, lengo ni kutumia mtandao huo kwa bei nafuu.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *