michezo

Haruna Niyonzima Kuhojiwa Simba

on

Haruna Niyonzima akiwa bado kwao Rwanda na kuchelewa kujiunga na kikosi cha Simba kwenye kambi ya Uturuki, Rais wa Simba Salim Abdallah amesema Niyonzima hatoweza tena kwenda Uturuki kwa sababu muda umekwenda.

Salim amesema wanatarajia kumhoji Niyonzima kwa kosa la kukaa kimya hadi sasa.

“Haruna ni mchezaji wa Simba, tulimpa ruhusa maalum ya mapumziko na matibabu kule kwao Rwanda.”

“Tarehe ambayo alitakiwa kurudi Haruna ilikuwa ni July 20 ili aweze kuungana na wenzake, hata passport yake ina visa ya Uturuki lakini kwa sababu ambazo tumeshindwa kuzifahamu hadi sasa Haruna hajajiunga na timu, mwaka jana alikosa pre-season hata performance yake haikuwa nzuri kwa sababu ya kukosa pre-season na kukaa pamoja na wenzake.”

“Mwaka huu tena anakutana na tatizo hilohilo, sisi kama uongozi tunajaribu kuangalia kwa nini Haruna hajajiunga na timu kwa ajili ya pre-season.”

“Zipo taratibu na namna ya kufanya, kama ni makosa basi tutamwadhibu kwa mujibu wa taratibu zetulakini tutampa nafasi ya kujieleza kwa nini hajajiunga na timu.”

“Inawezekana ikawa ni tabia yake lakini na sisi kama klabu tuna tabia yetu kwa hiyo hatuwezi kuiga tabia yake. Kama amekosea zipo taratibu za kuchukua, yule ni mchezaji inawezekana ana jambo linamsumbua tutamwita tutamsikiliza halafu tutaona ni kitu gani cha kufanya.”

“Kuhusu ishu ya kiwango, Haruna amekuwa na matatizo msimu uliopita, alikuwa na majeraha na ni kawaida mchezaji anapokuwa na majeraha kiwango kinateremka kidogo. Kwa hiyo msimu huu ndio wakati wa Haruna kupandisha kiwango chake.”

“Bado nasisitiza Haruna ni mchezaji mzuri na ana kiwango kikubwa cha kuisaidia Simba.”

“Hawezi kwenda tena Uturuki kwa sababu siku zimekwisha, nadhani hakuna mchezaji tena atakaekwenda Uturuki kuungana na klabu. Baada ya kumsikikiza na klabu kufanya maamuzi tutashauriana na mwalimu kuona kama mwalimu anaweza kumpa program maalum kufidia yale ambayo wamefanya wenzake.”

Chanzo: SportLeo @RadioOne

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *