habari

Hatimae maagizo ra Rais Magufuli kuhamia jengo lisilomaliza yafuatwa

on

 

Na Mwandishi wetu Dododma

Katika kile kilichokua kikishubiriwa na wengi hatimae  Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara amesema kuanzia jana Jumatatu Aprili 15, 2019  wizara hiyo imehamia hivyo hivyo katika jengo la ofisi yake  ‘pagale’ ambayo haijakamilika kama ilivyoagizwa na Rais John Magufuli.

Waitara ametoa kauli hiyo leo nje ya viwanja vya Bunge jijini Dodoma zikiwa zimepita siku tatu tangu Rais Magufuli kutoa agizo hilo wakati akizindua mji wa Serikali jijini Dodoma

Rais Magufuli alitoa agizo hilo ikiwa ni muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kueleza kuwa alikuwa na makubaliano na mawaziri kuwa siku majengo hayo yakizinduliwa mawaziri wangehamia.

Hata hivyo Majaliwa alimweleza Rais kuwa kuna baadhi ya wizara ikiwemo Tamisemi ambazo majengo yao yamechelewa kukamilika kutokana na kuchelewa kupata fedha.

Akizungumzia agizo hilo Waitara amesema wameshamia umeshahamia tangu jana kwa mujibu wa maelekezo na ofisi za wizara hio zipo wazi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *