michezo

Hatma Ya Msimu Wa Liverpool Hutegemea Wiki Hii.

on

MSOMAJI, Liverpool wamekuwa na msimu mzuri, wamefikia fainali ya Ligi ya Mabingwa, Mohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora katika EPL na kocha wao Jurgen Kloop anawania tuzo ya kocha bora wa msimu nchini England.

Hata hivyo, Liverpool wapo katika hatari ya kupoteza kazi kubwa na mafanikio ambayo wameyapata msimu huu. Liverpool wana lengo la kupiga hatua kubwa zaidi kila msimu. Na katika miaka zinazokuja ni muhimu sana kwa klabu hiyo kuendelea kushiriki katika Ligi ya Mabingwa.

Ni kwa kuwa mashindano hayo yanasaidia uchumi ya vilabu vingi kutokana na kila klabu kupata fedha nyingi kila hutua wanao ivuka katika Ligi ya Mabingwa. Lakini, muhimu zaidi ni kwamba wachezaji bora duniani wanataka kucheza katika Ligi ya Mabingwa na hivyo ni rahisi zaidi kwa klabu ambayo inashiriki katikia michuano hayo kusajili wachezaji wenye vivango vikubwa.

Kwa idadi kubwa ya msimu kumekuwa na ishara nyingi kwamba Liverpool watafinikiwa kunasa moja ya nafasi nne za juu katika Ligi Kuu na kufuzu kushiriki katika Ligi ya Mabignwa msimu ujao pia. Lakini, katika takriban mwezi mzima sasa Liverpool wameshindwa kupata matokeo katika Ligi Kuu ya England.

Wikiendi iliyopita walifungwa na Chelsea na katika mechi zao tano za mwisho wameshinda mechi moja tu. Liverpool watacheza mechi yao ya mwisho katika Ligi Kuu wiki hii. Ni mechi ya nyumbani dhidi ya Brighton. Wakishindwa kushukuwa pointi tatu basi kuna uwezekano kwamba wataishia katika nafasi ya tano kama Chelsea wanashinda mechi zao mbili za mwisho dhidi ya Hudersfield na Newcastle.

Hakika sababu moja ya Liverpool kupoteza pointi nyingi katika Ligi Kuu katika wiki za hivi karibuni ni kutokana na kocha wa timu hiyo kupumzisha wachezaji wengi katika mechi za Ligi Kuu kabla mechi za Ligi ya Mabingwa.

Lakini pia kuna ishara kwamba wachezaji wa Liverpool wameshoka. Katika mfumo wa Kloop wachezaji wote huhitaji kujituma na kukimbia sana. Na kutokana na Liverpool kutokuwa na kikozi kipana sana wachezaji kama Mohamed Salah, Sadio Mane, na Firmino wamecheza katika takriban mechi zote.

Hivyo sio jambo ya kushangaza sana kwamba hali yao ya kimpira imeshuka kidogo katika mechi za hivi karibuni katika Ligi Kuu.

Bila shaka Liverpool bado wana nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa hata kama wanaishia katika nafasi ya tano katika Ligi Kuu kama wanashinda Ligi ya Mabingwa kwa kuwa mshindi wa mashindano hayo anafuzu moja kwa moja kushiriki katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Hata hivyo, nafasi za Liverpool kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa kuwafunga Brighton katika mechi yao ya mwisho ni kubwa kuliko klabu hiyo kuifunga Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa. Hivyo, huenda hatima ya msimu wa Liverpool upo katika mechi yao dhidi ya Brighton wikiendi hii.

-Mwisho-

Na Olle Bergdahl Mjengwa

About Innocent Chambi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *