habari

Hoja ya kubenea kutaka Z’bar iruhusiwe kukopa nje ya Nchi yakwama

on

 

Na Mwandishi wetu Dododoma

Katika kile kilichoonekana kuibua hamasa kwa wabunge wengi jana mjini Dodoma ni baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea jana jioni kutoa katika ukumbi wa jengo hilo akitaka Serikali itamke lini itapeleka bungeni marekebisho ya Katiba na sheria ili kuiruhusu Zanzibar iweze kukopa nje kwa ajili ya kuendesha miradi yake mikubwa.

Kubenea ametoa hoja wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha kifungu kwa kifungu cha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais  ya mwaka 2019/2020 ambayo ni Sh 36 bilioni.

Hoja ya Mbunge huyo aliungwa mkono na wabunge wengi waliochangia hoja yake hiyo ambayo ilitolewa ufafanuzi mara mbili na naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashantu Kijaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi huku mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akitumia nafasi yake kuwatuliza wabunge.

“Katika hoja hio kubenea aliuliza Serikali ni  italeta muswada ili kuifanya Zanzibar iweze kukopa kutoka mataifa ya nje kama ilivo Tanzania bara hoja ambayo ilijadiliwa na wajumbe wengi w aBunge hilo.

Akitoa ufafanuzi wake Dk Kijaji amesema kuwa mambo mengi yapo kwenye mchakato wa majadiliano katika ngazi ya wataalam na sasa yamekamilika, tunaandika waraka wa baraza la mawaziri mambo hayo yaweze kupatiwa ufumbuzi na tiba ya kudumu.”

Hata hivyo alimtaka Mbunge huyo na wengine kuvuta  subira Serikali ina dhamira kuhakikisha kero zote za muungano zinaondoka, kuwekwa kwa mfumo huu jinsi ulivyo upo kisheria tutakuja kutoa majibu hapa hapa.

Akifafanua suala hilo Profesa Kilangi alisema kwamba , Mikopo ni suala la muungano kwa mujibu wa katiba hivyo watakapkua wakumbe kwamba jambo hilo limelezwa kwa misingi ya kikatiba.

Akiendelea kutoa ufafanuzi wa maelezo ya Profesa Kilangi na Dk Kijaji, Kubenea amesema anajua kwa mujibu wa Katiba yameorodheshwa mambo ya muungano, “Serikali iseme lini mchakato wa kubadilisha Katiba na Sheria yake. Waziri anasema tutaleta tupo katika majadilino, natoa shilingi ili wenzangu waniunge mkono tujadili jambo hili kwa mapana zaidi.

Wabunge wachangia

Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Antony Komu aliunga mkono hoja ya Kubenea na kubainisha kuwa miaka 55 tangu muungano wa Tanganyika na Zanzibar  mambo hayo yamekuwa yakizungumzwa, imekuwa ikiahidiwa kuletwa bungeni lakini hayaletwi jambo alilodai linahatarisha muungano.

“Tunafikiri Zanzibar ipewe fursa ya kujisimamia na kukopa maana vipaumbele vya Serikali ya muungano si vya Zanzibar, Zanzibar ina vipaumbele vyake kwa ajili ya ustawi wa watu wake, sasa kwa ajili ya vikwazo  mambo hayo hayawezi kufanyika kwa sababu ya kikwazo hiki kilichopo katika katiba,” amesema Komu.

Kwa upande wake mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema, “Serikali iseme lini italeta muswada wa sheria ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kuiruhusu Zanzibar kuingia mikataba ya mikopo na misaada ya kimataifa bila kutegemea dhamana au kuruhusiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”

“Maelezo ambayo Serikali inayatoa kulingana na mchakato ni maelezo ambayo hayaaminiki. Mwaka 1977 Katiba ibara ya 134 ilianzisha Tume ya pamoja ya fedha, ilichukua mpaka mwaka 1996 Serikali ya CCM kuleta muswada wa tume hiyo ya pamoja ya fedha, ilichukua tena mpaka 2003 Serikali  ikaleta kanuni ya kuitekeleza hiyo sheria.”

Ameongeza, “Mpaka sasa tume haijaanza kufanya kazi. Uchambuzi uliofanywa na tume ya pamoja ya fedha inaonyesha yanayopaswa kugawanywa pande zote mbili za muungano yanatumiwa na Tanzania Bara na Zanzibar haipati hata senti tano.”

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayoub amesema  Zanzibar uchumi wake mdogo na inategemea zao la karafuu, “sasa inataka kukua na kuendelea mbele na inalia na kuendeleza bandari ya Mpigaduli na uwanja wa ndege.”

“Lini  mseme kama ni miezi sita au mwaka mmoja. Mtu akilia kuna jambo tufikilieni jamani. Naungana na Kubenea asilimia 95 tufikilieni jamani,” amesisitiza Jaku.

Akichangia jambo hilo mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene amesema,”Niseme tu kwamba yapo mambo makubwa na miradi mikubwa iliyofanyika nchi hii kwa ushirikiano wa Serikali zote mbili, kusema kuna tatizo kubwa la mikopo naweza kusema sawa, lakini yapo mambo makubwa yamefanyika. Takwa la sheria linaloombwa na Kubenea kuleta sheria hapa si jambo dogo ni mabadiliko ya katiba.”

Kubenea alivokataa maelezo

Kubenea aliporejeshewa kumaliza hoja yake amesema, “anapozungumza waziri kuhusu dhamana inatolewa na Benki Kuu, na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina share katika benki kuu ya Tanzania ndio maana inapata gawio pale benki kuu inapopata faida.”

Hata hivyo alisema alitegemea Serikali baada ya miezi mitatu ingesema italeta jambo hili, tunataka marekebisho ya sheria ili Serikali ya Zanzibar iweze kukopa nje. Naomba Bunge hili lihojiwe wangapi wanakubali hoja yangu na lini Serikali italeta mabadiliko ya sheria na katiba.

Licha ya mivutano mikali ya hoja kwneye bunge hilo hatimae wabunge walihojiwa iwapo wanakubali au kukataa hoja hio lakini waliokataa walikua wengi na kupelekea hoja hio kutopitishwa.

 

 

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *