siasa

Humphrey Polepole “Tunataka Aeleze Hiyo Sh 1.5 Trilioni Kaipata Wapi, Alizua Taharuki”

on

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amesema Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe hajui hesabu kwa kuwa hakuna fedha iliyopotea hivyo amemshauri amtafute mtaalam wa hesabu.

Polepole amesema hayo leo Jumatano Aprili 18 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

“Huyu ni muongo alianza na santuri ya njaa akatangaza nchi ina njaa. Tumezunguka nchi nzima hakuna njaa, akaona haitoshi akamgeukia rais wetu kuwa ni dikteta wakati yeye anaendesha chama kupitia Facebook.” Alisema Polepole.

“Kuna wakati anasema kamati kuu imekaa kumbe uongo anaandika facebook”

“Niombe uongozi wa Bunge wakati mwingine uwe unawabana wabunge wawe wanathibitisha mambo wanayoyazungumza bungeni.”

“Wenye dhamana ya kusimamia sheria wachukue hatua, kucheka cheka na mizaha kwa kauli hizi haivumiliki. Tunataka aeleze hiyo Sh 1.5 trilioni kaipata wapi, alizua taharuki, nasisitiza tusimuache alizoeshwa vibaya huyu maana tunajua sisi ndio tupo kwenye chama.”

Na Mwananchi.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *