habari

Idadi Ya Waliouawa Afghanistan Yaongezeka.

on

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kujitoa muhanga imeongezeka na kufikia Takribani watu  57. Taaarifa za awali ziliripoti kuwa watu waliopoteza maisha walikuwa 31, lakini idadi hiyo imeongezeka kutokana na hali mbaya waliokuwa nayo majeruhi wa tukio hilo, lililotokea mjini Kabul, ambapo mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijiripua kwenye kituo cha kuwasajili wapiga kura.

Shambulio hilo limefanyika baada ya siku kadhaa za utulivu katika mji huo. Watu wengine zaidi ya mia moja walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Mauaji hayo, yanaelezwa kuwa yanaweza kuchelewesha uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika terehe 20 mwezi Oktoba.

Kundi la magaidi wanaojiita dola la Kiislamu (IS) wamedai kuhusika na shambulio hilo na hivyo kuongeza wasi wasi mkubwa juu ya usalama kabla ya kufanyika uchaguzi huo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *