habari

Idara Ya Uhamiaji Yaweka Utaratibu Kwa Raia Wa Burundi Wanaotaka Kuja Nchini.

on

Idara ya Uhamiaji nchini imeweka utaratibu wa kutoa kibali maalum kwa raia wa Burundi, watakaohitaji kuja nchiniTanzania kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo ikiwa ni moja ya njia za kupunguza raia wa nchi hiyo ambao huingia kinyemela hususani katika mikoa ya Kigoma na Tabora, kwa ajili ya kufanya kazi za kilimo kama vibarua.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Anna Makakala ametangaza mpango huo mwishoni mwa ziara yake iliyomfikisha katika wilaya zote na katika maeneo ya mpaka na nchi jirani, ambapo amesema kuwa vibali hivyo vya miezi mitatu vitawezesha raia wa Burundi kutambuliwa na serikali, kupata fedha na kutambua wako wapi pamoja na idadi yao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema uamuzi huo wa idara ya uhamiaji, utasadia katika kupunguza uhalifu na kuongeza tija katika kilimo, pamoja na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani ya Burundi, ambayo raia wake wanaongoza kwa kuja nchini kufanya vibarua bila ya kibali na hivyo kuongeza idadi ya wahamiaji haramu.

Na Dar24.com  http://dar24.com/raia-wa-burundi-walamba-dili-tanzania/

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *