habari

ILO: Watu Bilioni 2 Wapo Katika Ajira Zisizo Rasmi.

on

Wakati dunia inaadhimisha sikukuu ya wafayakazi, Shirika la Kazi duniani ILO limetoa ripoti inayoonyesha kuwa katika watu Bilioni 2, sawa na asilimia 61 ya watu walioajiriwa, wapo katika ajira zisizo rasmi.

Ripoti hioyo inaeleza pia kuwa, watu hao wanatoka katika mataifa yanayoendelea kiuchumi, huku wanawake wakiwa ni Milioni 740.

Barani Afrika, asilimia 85.8 ya ajira sio rasmi huku  bara la  Asia likiwa katika nafasi ya pili kwa asilimia 68.2.

Aidha, ripoti inaeleza idadi kubwa ya watu wanaojihusisha katika ajira hizo sizozo rasmi ni wanaume, huku wanawake wakiwa ni asilimia 58.1.

Inaelezwa kuwa, kazi nyingi zilizo rasmi zinafanywa na watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini. Pamoja na hilo ukosefu wa elimu kwa watu wengi pia inachangiwa pakubwa kutokana na hali hii.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *