habari

Iran Yakosoa Kufungwa Kwa Mtandao Wa Telegram.

on

Rais wa Iran Hassan Rouhani amekosoa kufungwa kwa mtandao maarufu wa kutuma ujumbe wa Telegram katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu, kwa kusema utawala wake haukuhusika na kufungwa kwa mtandao huo.

Telegram inayoaminika kutumika na nusu ya idadi ya raia wa Iran milioni 80 ilihusika pakubwa katika kuchochea maandamano ya nchi nzima mwezi Desemba na Januari. Uongozi uliufunga mtandao huo kwa muda ili kutuliza maandamano ila mahakama ya Iran siku ya Jumatatu iliamuru kampuni zinazotoa huduma za intaneti kuufunga kabisa. Kutoka wakati huo watumiaji hawajaweza kuutumia.

Na sasa katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Rouhani amesema hakuna mtandao wa kijamii wala mtandao wa kutuma ujumbe uliofungwa na serikali yake na wala hakuna utakaofungwa.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *