We have 121 guests and no members online

Znateli
×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Zijue faida za domain ya .co.tz badala ya .com

Posted On Tuesday, 26 May 2015 10:44 Written by
Rate this item
(0 votes)

Website Hosting and Domain Registration in Tanzania

Ni mara ngapi umekuwa ukiumiza sana kichwa kwa sababu majina yote ya .com yanayoendana na jina halisi la biashara yako tayari yameshachukuliwa? mfano, wewe kampuni yako inaitwa Dudumizi, na kila ukitafuta dudumizi.com , Dudumizi.net na hata Dudumizi.info unakuta tayari yameshachukuliwa, hakuna sababu ya kuchanganyikiwa, tunayo .co.tz, majina ya kitanzania zaidi.

Watu wengi wamekuwa wakipendelea kutumia majina ya .com. Wengi wamekuwa na imani kuwa kwa kutumia majina ya .com kinawafanya waonekana kimataifa na kitaalamu zaidi, ingawa hili lina ukweli wake kiasi fulani, ila kwa upande mwingine, inategemeana sana na aina ya biashara unayoifanya na mlengwa mkuu wa biashara husika, majina ya .co.tz nayo yana faida tele kwa baadhi ya mazingira.

Kuna faida nyingi sana za kutumia majina ya kinchi (kama .co.tz) haswaa pale ambapo walengwa wako wakuu ni ndani ya nchi hiyo.Hebu tuangalie faida kadhaa zinazopatika kutokana na kutumia majina ya .tz

Mitambo ya utafutaji (Search Engines)

Search Engines huzipa upendeleo wa kipekee website zenye majina yaliyo ndani ya nchi ya mtafutaji, kwa mfano, kama mtu anatumia Google kutafuta wanaotengeneza Website Tanzania, basiDudumizi.co.tz itapewa kipaombele zaidi kuliko Dudumizi.com.

Kumbuka, matokeo ya utafutaji, pia huzingatia vitu vingine vingi, hivyo jina pekee si kigezo cha kukufanya uwe nafasi ya juu.

Uaminifu kwa watumiaji.

Je umeshawahi kujiuliza, pindi mteja anapotafuta duka au website ya kununua nguo, akaonana na website nguo.com na nguo.co.tz ni ipi itampa uaminifu zaidi? Ni dhahiri kuwa, nguo.co.tz inatoa imani zaidi ya nguo.com.

Pia, kutokana na mfumo wa usajili wa majina ya website, usajili wa majina ya kinchi huambatana na utambulisho ama wa msajili (registrar) au msajiliwa (Domain Owner), hii siyo tu husaidia kuongeza imani kwa watumiaji, bali pia thamani ya majina ya website.

Hivyo, pindi unapotaka kusajili majina ya .tz, basi usisite kutembelea wavuti ya tzNIC (taasisi inayohusika na uchungaji wa majina yote ya .tz) na kujihakikishia kama huyo msajili yupo kwenye orodha wa wasajili wa tzNIC.

Ingawa, mara nyingi huwa tunashauri kama unaweza, basi upate majina yote mawili, lile la nchi (mfano .tz) na .com. Baada ya hapo utaziunganisha (direct) ili ziweze kufanya kazi pamoja.

Jinsi ya kupata majina ya .tz

Kuna njia nyingi za kupata majina ya .tz, moja ni kwenda tzNIC na kupitia kwenye orodha ya wasaliji waliohidhinishwa na tzNIC, pia unaweza kwenda moja kwa moja Dudumizi.net na kutafuta jina lako na kununua papo kwa hapo.

Read 1019 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart