We have 213 guests and no members online

Znateli

AIRTEL NA HUAWEI YAANZISHA BAZAAR LA SIMU ZA SMARTPHONE.

Posted On Thursday, 04 June 2015 17:13 Written by
Rate this item
(0 votes)

Meneja Masoko wa Huwawei Bi Aneth Muga akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu aina ya Huwawei Met 7 ambayo zitauzwa katika Airtel Bazaar linalofanyika mlimani City ijumaa, jumamosi, na jumapili hii ikiwa na ofa ya simu ya bure aina ya 'Huwawei Kishkwambi' iliyoshikiliwa na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga. Pia simu hiyo itaunganishwa na ofa kabambe ya kifurushi cha Airtel papo hapo.

Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanahabari (hawapo pichani) simu ya kisasa ya Airtel Red itakayopatikana kwa gharama nafuu katika Airtel Bazaar litakalofanyika wiki hii ijumaa, jumamosi, na jumapili hii pale mlimani City kwa gharama nafuu huku ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha Airtel bure. Anaetazama ni Meneja Masoko wa Huwawei Bi Lydia Wangari.

Na Mwandishi wetu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania ikishiriakiana na Huawei leo imetangaza kuanza Bazaar lake maalum litakalowawezeha watanzania kujipatia simu za kisasa za Smart phone na kuweza kufurahia huduma za zote za intaneti kupitia mtandao wa Airtel

Bazaar la Airtel na Huawei limepangwa kufanyika kuanzia ijumaa, jumamosi na jumapili hii kuanzia saa 3asubuhu hadi saa moja usiku katika eneo la ndani la Mlimani City na litakuwa na muendelezo hapohapo na baadae litazunguka katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumzia Bazaar hilo Meneja masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema "Bazaar letu litakuwa la kijanja zaidi kwani simu za smart phone zitakazouzwa ni bora na zitaambatana na ofa kabambe kuliko zote zinazopatikana sehemu yoyote".

"Mteja wetu uliopo mahali popote tembelea BAZAAR la Airtel ujinyakulie simu bora na kisasa kama zile za Huawei au Airtel Red kwa punguzo kabambe zikiwa na kifurushi cha intaneti kitakachokupa MB 120, SMS 120 pamoja na muda wa maongezi 120 ofa ambapo huwezi kuipata popote zaidi ya kweye Airtel Bazaar" alisema Muga 

Meneja masoko kutoka Huawei Lyidia Wangari aliongeza kuwa licha ya simu za Smart phone za Huawei kuuzwa kwa gharama nafuu pia atakaenunua simu pale atajipatia simu nyingine ya bure au zawadi tofauti tofauti papo hapo kwa mfano "mteja yeyote kati ya 300 wa kwanza kununua simu ya Huwawei aina ya Met 7 DUAL atapata simu aina ya Kishkwambi bure kabisa na atakaenunua simu ya Huawei Met 7 atapata simu ya bure aina ya Y220 pale pale" alifafanua

Kwa Upande wake Afisa Airte l wa kitengo cha Smartphone Bw, James Kagashe alisema "tunataka kudhihirisha kwa wateja wetu kuwa Airtel ndio mtandao sahihi kwa Smartphone yako popote ulipo, nakuhakikishia kuwa kila simu inayouzwa katika Artel Bazaar inakuja na ofa kabambe ya kifurushi cha SMS, dakika za muda wa maongezi pamoja na intanet itakayokuwezesha kuperuzi upendavyo"

Nawahamasisha wale wote mnaotaka kuenda na wakati kwa kumiliki simu bora na kuunganishwa na mtandao bora kwa Smartphone yako tembelea Airtel Bazaar la Airtel Mlimani City ili tukuunganishe. Alimaliza kwakusema Bw Mwanda. (Muro)

Read 1811 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart