We have 362 guests and no members online

Smart

MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA MBULU AKAGUA UJENZI WA MIUNDOMBINU SHULE YAEDA CHINI MBULU

Posted On Friday, 26 January 2018 06:22 Written by
Rate this item
(0 votes)

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Diwani kata ya Yaeda Chini (CCM) Bryson, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea Tsh 281,500,000 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga. Fedha hizi ni sehemu ya Zaidi ya Tsh 17 Bilioni zilizotolewa na Serikali kwa baadhi ya Halmashauri nchini kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi na sekondari!

Ni lengo la Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dr. John Pombe Magufuli kuondoa kero katika sekta ya elimu nchini. Tumeshaanza maandalizi ya ujenzi na kukamilisha kwa wakati ufanisi wa hali ya juu katika shule hizo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu ,Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Faustine Safari kushoto, wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akiongozana na Afisa Elimu Wilaya ya Mbulu Ludovic Longino kulia na Afisa ugavi wilaya ya Mbulu Bw. Faustine Safari kushoto wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaeda Chini na shule ya Msingi Domanga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Wilaya ya Mbulu wakati Mkurugenzi huyo alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akishiriki katika ujenzi wa Msingi wa shule wakati alipokagua ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya shule ya sekondari Yaenda Chini na shule ya Msingi Domanga

Read 52 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli