We have 378 guests and no members online

Watumishi

WATU 95 WAPOTEZA MAISHA, 158 WAJERUHIWA VIBAYA AFGHANISTAN

Posted On Saturday, 27 January 2018 16:48 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la Deadly blast rocks Kabul

Watu 95 wamepoteza maisha na wengine 158 kujeruhiwa katika shambulio la kubwa la kigaidi katika mji mkuu wa Afghanistan -Kabul.

Kundi la kigaidi la Taliban limehusishwa kutekeleza shambulio hilo ambalo ni la tatu kutokea katika kipindi cha muda wa siku saba zilizopita.Washambuliaji katika tukio hilo wameripua gari la kubebea wagonjwa katikati ya mji wa Kabul nchini humo karibu na ofisi za serikali, shule, maeneo ya biashara na hospitali ya Jamhuriat.

Shuhuda mmoja aliyefahamika kwa jina la Ahmed Naweed, ameliambia shirika la habari la     Al Jazeera kwamba mlipuko huo umetokea kati ya vituo viwili vya ukaguzi, na muda mchache baadae kulikuwa na miili ya watu wengi katika maeneo mbalimbali pamoja za damu nyingi, huku mashuhuda wengine wakilia na wengine kukimbia.

Habari zaidi zinasema majeruhi wamepelekwa hospitali kupatiwa matibabu ingawa idadi ya watu waliopoteza maisha inahofiwa kuongezeka kutokana na kuumia vibaya baadhi ya majeruhi.

Tokeo la picha la Deadly blast rocks Kabul

Read 46 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli