We have 259 guests and no members online

Watumishi

WATU 7 WANUSURIKA KUFA MAJI BAHARI YA PACIFIC

Posted On Sunday, 28 January 2018 22:03 Written by
Rate this item
(0 votes)

Meli iliyokuwa na manusura (L) na meli ya uokozi katika bahari ya Pacific. Januari. 28, 2018.

Kikosi cha anga cha New Zealand kimewagundua Jumla ya watu sita akiwemo mtoto mmoja, waliokutwa wakiwa hawajitambui baada ya kuelea kwenye maji zaidi ya wiki moja katika boti ndogo ya mbao katika bahari ya Pacific.

Aidha kikosi hicho wakati kikiwatafuta manusura wa boti ambayo ilizama wakati ikisafiri kati ya visiwa viwili katika taifa hilo dogo la Kiribati,wafanyakazi wa kikosi cha anga walifanikiwa kudondosha vifaa ikiwemo maji na chakula kwa manusura hao.  Maafisa wa uokozi wanasema Boti ya MV Buritaoi ilibeba abiria 50 na iliondoka kisiwa cha Nonouti Januari 18 kwa safari ya siku mbili ikielekea South Tarawa. Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters, wafanyakazi wa dharura wa New Zealand waliambia kuhusu kupotea kwa boti hiyo siku ya Ijumaa ikiwa ni siku nane baada ya boti hiyo kuondoka bandarini.Kikosi cha anga cha New Zealand kinasema hakuna ishara ya kuwapata abiria 43 waliobaki.

Read 69 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu