We have 335 guests and no members online

Watumishi

AJALI YA MOTO KENYA, WATU WANNE TAYARI WAMERIPOTIWA KUPOTEZA MAISHA.

Posted On Monday, 29 January 2018 12:06 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la fire break in langata nairobi

Watu wanne wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya moto uliotokea usiku wa kuamkia leo January 29 katika mtaa wa Kijiji eneo la Langata-Nairobi, huku wengine wakiripotiwa kukesha baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto.

Kwa mujibu wa Maafisa wa serikali nchini humo, nyumba 6,000 makazi ya watu karibu 14,000 ziliharibiwa na moto huo.

Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja, Magari manne ya vikosi vya zima moto yalifika eneo hilo kujaribu kuuzima moto huo ingawa vikosi hivyo havikuweza kuuzima kutokana na njia za mtaa huo kuwa nyembemba na hivyo magari ya zima moto hayakuweza kupita.

Wananchi wa maeneo hayo ulikotokea moto huo, walipokuwa wakiongea vyombo vya habari wamesema walipoteza mali zenye thamani ya mamilioni ya pesa, huku baadhi wakipoteza biashara zao na wengine makazi.

Pius Masai ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Kukabiliana na Majanga anayeangazia mawasiliano, aliambia gazeti la kibinafsi la Nation kwamba walilazimika kuomba msaada zaidi wa Magari ya kuzima moto ya baraza la jiji, lakini wakazi waliwalaumu maafisa hao wa serikali kwa kuchelewa kufika eneo la mkasa.

Read 48 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli