We have 146 guests and no members online

Znateli

KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA ATEMBELEA CHUO CHA MUHIMBILI.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 10:05 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA CHUO CHA MUHIMBILI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii jinsia na watoto, Dk Mpoki Ulisubisya, amefanya ziara kwenye Chuo Kikuu cha Tiba ya Afya Shirikishi, Muhimbili University of Health Allied Science (MUHAS) ambapo mbali na mambo mengine, amezungumzia kuhusu mikakati ya serikali katika kuongeza wataalamu wa afya ili kuboresha huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali nyingine nchi nzima.

Pia amezisisitizia taasisi za afya kutosubuiri matatizo kutoka kwa wananchi kwani kusubiri mpaka wananchi walalamikie huduma za afya inaweza kuchukua muda mrefu katika kupata huduma za afya. Vile vile amesema kuna uhitaji wa kuzalisha zaidi wakunga katika ngazi ya shahada ya kwanza ili kupunzuza vifo vya akina mama wanaojifungua ambavyo kwa sasa vinakadiriwa kufukia 556 kati ya kinamama laki moja  wanaojifungua.

Read 45 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu