We have 131 guests and no members online

Znateli

RASMI AUBAMEYANG ASAINI MKATABA KUJIUNGA NA ARSENAL.

Posted On Wednesday, 31 January 2018 13:10 Written by
Rate this item
(0 votes)

Tokeo la picha la AUBAMEYANG

Mshambuliaji wa klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang leo ametia saini mkataba wa muda mrefu kuichezea klabu ya Arsenal.

The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette.

Klabu ya Arsenal imeandika kwenye mtandao wao kwamba Aubameyang ni Mchezaji wao wa pili kumnunua katika kipindi cha kuhama wachezaji mwezi Januari.

Aubameyang ni miongoni mwa washambuliaji stadi zaidi duniani ambapo amefunga mabao 98 katika mechi 144 akiwa kwenye klabu ya Dortmund inayocheza ligi ya Bundesliga na amesaidia ufungaji wa mabao 172 katika mechi 213 ambazo ameshiriki akichezea klabu hiyo.

Awali klabu ya Dortmund ilisema itamuuza mcheza huyo endapo tu itampata mbadala wake huku mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.

Tangu mwaka 2013 akiwa Dortmund Aubameyang amefunga mabao 141 katika mechi 213 zikiwemo mechi 21 kati ya 24 msimu huu.

Read 41 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart