We have 167 guests and no members online

Znateli

“HATUKUCHEZA KAMA TULIVYOTAKA” LWANDAMILA

Posted On Sunday, 11 February 2018 02:48 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for LWANDAMILA

Baada ya mchezo wa hapo jana dhidi ya St Louis ya Shelisheli, Kocha wa Yanga, George Lwandamina amekubali kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri kama walivyotarahia. Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Washelisheli hao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lwandamina ambaye ni raia Zambia, amesema anaamini wana nafasi ya kurekebisha makosa yao katika machi ya pili wakiwa ugenini na kufanya vizuri. “Hatukucheza kama tulivyotaka, tumejitahidi lakini bado tuna nafasi ya kujirekebisha na kufanya vizuri,” alisema. Lwandamina alilazimika kufanya mabadiliko mwishoni mwa kipindi cha pili ili kupata bao baada ya washambuliaji wake wawili, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kushindwa kuonyesha cheche ikiwa ni pamoja na kukosa penalti.

Read 67 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu