We have 149 guests and no members online

Simu

MCL yaongoza kwa kuwania Tuzo MCT

Posted On Thursday, 30 January 2014 04:24 Written by
Rate this item
(0 votes)

kajubi ec130

Gazeti la Mwananchi kwa mara ya pili mfululizo waandishi wake wameongoza kwa kupeleka kazi nyingi zaidi ya vyombo vingine vya habari katika Shindano la Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2013. (HM)

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana kabla ya kuapishwa kwa majaji tisa ambao watawachagua washindi wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo hizo, Kajubi Mukajanga alisema, jumla ya kazi 907 za 2013 zimepokewa.

Alisema magazeti ndiyo yameongoza kwa kuwa na kazi 638 zikiwa ni pungufu kulinganisha na kazi 660 za 2012, gazeti la Mwananchi likiwa linaongoza kwa kuingiza kazi 233 ambazo ni zaidi ya 204 za mwaka 2012 na kufuatiwa na gazeti la The Guardian (99) na Business Times (91).

Magazeti ya Daily News na Habari Leo (49), TBC (65) na Afya Radio (44), kwa mujibu wa Mukajanga, vyombo vya elektroniki vimeshika nafasi ya pili kwa kuingiza kazi 269 na kufautiwa na Radio (165), televisheni (104).

"Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa waandishi wake kupeleka kazi 500 na kufuatiwa na Mwanza (103), Arusha (59), Zanzibar (57) Kagera (23) na kwa mara ya kwanza habari za uchunguzi zitashindanishwa,"alisema Mukajanga na kuongeza kuwa, waandishi wengi wametuma kazi zaidi ya moja tofauti na wakati uliopita.

Alisema katika hafla hiyo ya utoaji wa tuzo inayotarajiwa kufanyika Machi 14, mwaka huu, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jaji Harold Nsekela. Chanzo: mwananchi

Read 1416 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji