We have 546 guests and no members online

BCU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.

Posted On Monday, 20 March 2017 16:15

BVCCCCCCCCCCCCCCC

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameunda kamati ya watu watano kuchunguza suala la kilichotokea Clouds Media siku ya Alhamisi pamoja na Ijumaa usiku.

Posted On Monday, 20 March 2017 16:14

BUGU

Katibu  wa Bunge ambaye pia ni msimamizi wa Uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Thomas Kashililah  akizungumza na wawakilishi mbalimbali wa Vyama vya Siasa kuhusu uchaguzi wa Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashiriki. Wa kwanza kulia kwake ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Posted On Monday, 20 March 2017 16:11

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Mizan al haq ina maana ya mizani ni haki. Ndio maana, hata alama kuu ya mahakama ni mizani.
Asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Mkulima anategemea mzani ili uamue uzito halisi wa ujazo wa mazao yake.

Lakini, ni mzani ndio umechangia kumdidimiza mkulima wa Tanzania. Wafanyabiashara wengi wenye kutumia mizani katika kununua mazao ya mkulima wamekuwa wakifanya hila na mizani hiyo.

Pichani ni Zanzibar, jana asubuhi.

Maggid.

Posted On Monday, 20 March 2017 04:32

media

Damascus, Machi 19, 2017. Moshi mkubwa katika eneo la Jobar, mashariki mwa mji mkuu wa Syria unaokumbwa na mapigano makali

Posted On Monday, 20 March 2017 04:30

dun1

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Mshauri Mwandamizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia nchi 21 Kanda ya Afrika Bw. Wilson Toninga Banda, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Yong Kim.

Posted On Monday, 20 March 2017 04:27

Bi.Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, mmoja wa wagombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki akikabidhiwa fomu na  Bw. Said Bakari wa  Idara ya Uhusiano wa kimataifa katika makao makuu ya CCM mtaa wa  Lumbumba jijini Dar es salaam.

Posted On Monday, 20 March 2017 04:23

 Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (wa pili kulia), akimkabidhi moja ya jaketi angavu (Reflector Jacket) kati ya majaketi 500 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda katika hafla iliyofanyika wilayani humo jana. LAPF imetoa majaketi hayo kwa ajili ya kusaidia waendesha bodaboda ili waweze kutambulika wakiwa katika shughuli zao za kila siku.Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfumo wa Uchangiaji wa Hiari wa LAPF, Hanim Babiker, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, William Gama na Meneja wa LAPF, Kanda ya Mashariki,  Lulyalya Sayi. 

Posted On Monday, 20 March 2017 04:22

chin

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Youqing, nyumbani kwa Balozi huyo, jijini Dar es Salaam, jana, Machi 19, 2017. Mazungumzo hayo yalihusu zaidi kuhusu juhudi za kuongeza ushirikiano baina na CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhusiano wa kidundugu uliopo kwa siku nyingi baina ya vyama hivyo na uchumi. (Picha na Bashir Nkoromo).

Posted On Monday, 20 March 2017 04:17

ki1

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw. Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini  Mauritius kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Posted On Monday, 20 March 2017 04:11

 Balozi wa Tanzania Mhe. Philip Marmo na  Acting Colonel Joseph Bakari wakisikiliza maelezo kabla ya hatua ya kumvua cheo cha zamani na kumvika kipya

Posted On Monday, 20 March 2017 04:06

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akiendeseha baiskeli hiyo kabla ya kumkabidhi mkazi wa Makorora Mbwana Hamisi jana kwa ajili ya matumizi yake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande 

Posted On Monday, 20 March 2017 04:01

maj1

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Leonardo Mloe akitwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama baada ya kutembelea mradi wa maji ZOJOSA  huko kata ya Misugusugu (picha na Mwamvua Mwinyi)

Posted On Monday, 20 March 2017 03:59

sa1

 Baadhi ya Watumishi wa shirika la nyumba mkoa wa Arusha wakimsikiliza Naibu waziri Mabula alipotembelea na kukagua nyumba zinazojengwa na shirika la nyumba hapo (PICHA NA MUUNGANO SAGUYA-NHC)

Posted On Monday, 20 March 2017 03:52

mbo1

Kamishna msaidizi, kanda ya ziwa; Joseph Shewiyo akisoma taarifa ya Utekelezaji ya kanda ya ziwa, mkoani Mwanza.

Posted On Sunday, 19 March 2017 07:24
Page 8 of 1944

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart