We have 954 guests and no members online

nga1

Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba  (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la  kufanya mazoezi, kupima afya,kuchangia damu,leo jijini Dar es Salaam katika  ulioshirikisha Jukwaa la Wahariri (TEF) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam. Tamasha hilo litafanyika siku ya Jumamosi  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  Kuotoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil na Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein.

Posted On Wednesday, 15 February 2017 16:24

jap1

Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Roxana Kijazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

Posted On Wednesday, 15 February 2017 16:22

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto), akipongezwa na Kamishna  Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi  (kulia) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro baada ya kuchaguliwa Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA  NA RICHARD MWAIKENDAKAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Posted On Wednesday, 15 February 2017 16:12

media

Mazungumzo baina ya Burundi yalizinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.

Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa, anatazamiwa kujaribu tena kuleta pamoja serikali na upinzani kwenye meza moja ya mazungumzo kuanzia Alhamisi hadi Jumamosi wiki hii mjini Arusha (kaskazini mwa Tanzania), mchakato ambao unaonekana kutozaa matunda yoyote.

Posted On Wednesday, 15 February 2017 16:05

MAJALIWA MCHANGO MADAWATI CUE IN

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wawe wabunifu katika kusaidia kutafuta vyanzo vya mapato kwenye jamii inayowazunguka.

Ametoa wito huo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) ofisini kwake mjini Dodoma mara baada ya kupokea mchango wa sh. milioni 5.6 kwa ajili ya kununulia madawati 70 kutoka kwa watumishi wa TAMISEMI – Dodoma.

Posted On Wednesday, 15 February 2017 03:12

KIDAA

Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya  BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma  mbalimbali za matibabu ya moyo ya  bila kufungua kifua (Catheterization).

Posted On Wednesday, 15 February 2017 03:05

UTI

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla akifungua Mkutano wa siku tatu wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na maradhi ya Polio Tanzania katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resourt Mbweni.

 UTI 1

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na Polio wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.

Posted On Wednesday, 15 February 2017 02:52

kemiA

Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mafunzo ya wasafirishaji na watumiaji wa Kemikali nchini, kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Everlight Matinga na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali nchini,Sabanitho Mtega, (kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, David Elias pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Biashara,George Kasinga.

Posted On Tuesday, 14 February 2017 10:25

CONGO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Gavana wa Lubumbashi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Claude Kazembe kuhusu mipango endelevu ya matumizi mazuri ya Bandari ya Dar es Salaam ofisini kwake jijini Dar es salaam.

CONGO 1

Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng, Deusdedit Kakoko leo, jijini Dar es salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Posted On Tuesday, 14 February 2017 07:18

mako2

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Siangakamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya  ili yaanze kushughulikiwa amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete  na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukubi wa Mwalimu Nyerere JNCC

Posted On Tuesday, 14 February 2017 03:47

ZIME

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Kassim Ali (wa pili kulia) wakati alipotembelea majengo ya Ofisi za Tume hiyo leo Maisara Mjini Unguja. 

ZIME 1

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Msaidizi Afisa Mawasiliano Mwanakombo Abuu Machano  wakati leo alipotembelea majengo ya Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilizopo  Maisara Mjini Unguja. 

Posted On Tuesday, 14 February 2017 03:44

POLIKO

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-

Posted On Tuesday, 14 February 2017 03:40

mkemia

Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Profesa Samwel Manyelle akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya taasisi hiyo Ocean Road wakati alipotoa taarifa ya mafunzo kwa wadau wa wanaoshughulika na mambo ya kemikali kulia ni Bw. Sabanitho Mtega Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti Kemikali.

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali  iliyo chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imekuwa ikitekeleza moja ya majukumu yake ambayo ni Sheria Namba 3 ya Udhibiti na usimamizi wa Kemikali za Majumbani na Viwandani ya mwaka 2003 . Lengo kuu la Sheria hii ni kulinda afya ya jamii na mazingira dhini ya kemikali.

Katika kutekeleza Sheria hii, Wakala hufanya Usajili na ukaguzi kwa wadau wote wanaohusika na kemikali wakiwemo waagizaji (Importers), Watengenezaji, (Producers) Wasafirishaji (Transporters), Watumiaji (users), Wanaosafirisha nje ya nchi (Exporters)  au yeyote yule anayehusika na kemikali kwa njia moja au nyingine. Pia ukaguzi unaohusisha mahali kemikali zinakotumika, zinakotunzwa au kuhifadhiwa (premises) unafanyika kila wakati.

Posted On Tuesday, 14 February 2017 03:35

LIMA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.

 LIMA 1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.

Posted On Tuesday, 14 February 2017 03:28
Page 9 of 1915

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart