We have 276 guests and no members online

A

Daktari bingwa wa upasuaji wa  Moyo  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hussein Hassanali (kulia) kwa kushirikiana na mwenzake wa Taasisi ya Healing Little Heart ya mjini London nchini Uingereza Ramana Dhannapuneni (kushoto) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha mlango wa moyo ambao unamatatizo na kumuwekea mwingine leo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa sita wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.

Posted On Friday, 07 April 2017 06:16

A 1

Mkurugenzi Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo utafanyika tarehe 11 mwezi April katika Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka  Hatibu.

Posted On Friday, 07 April 2017 06:13

media

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema kuwa Waziri Mkuu mpya anatarajiwa kuteuliwa kwa muda wa saa 48 zijazo.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:22

ccc

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Wazee wa Viongozi wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakati alipowasili katika majengo ya Skuli ya Sekondari ya Mohammed Juma Pindua Mkanyageni kuzungumza na wanafunzi wa skuli hiyo wa kuwapatia vifaa kwa ajili ya matumizi yao. ya kila siku skulini hapo.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:18

pic+ccm 

Na Mahmoud Ahmad Arusha

MAGEUZI ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi,pamoja na kanuni zake   yanalenga  kukidhi mahitaji ya sasa ya CCM mpya  na Tanzania mpya kwa kuteremsha madaraka ngazi za chini kuliko na wanachama  ili kukimarisha chama .

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:16

A

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:14

NEWSPAGES_20151012084243

Na Mahmoud Ahmad Kondoa,

Mgogoro umeibuka baina ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini na kampuni ya Kidee Mining(T) Ltd katika eneo la Tumbelo kata ya Kondoa mjini baada ya wachimbaji hao kulalamikia hatua ya kutaka kuondolewa kinyemela katika eneo hilo ili kuipisha kampuni hiyo.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:13

1

Ndugu, jamaa na marafiki hii leo jumatano April 05,2017 wameuaga mwili wa marehemu Profesa Lloyd Manamba Binagi aliyefariki ghafla juzi jumatatu April 03,2017 Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:10

DSCN7463

Tanga, KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:05

Z

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Charles Majinge akizungumza katika warsha kuhusu upasuaji wa matundu madogo bila kufungua tumbo iliyofanyika kwenye hospitali hiyo leo. Daktari bingwa aliyebobea katika upasuaji huo, Profesor Rafique Parkar kutoka Kenya ni mmoja wa watoa mada kwenye warsha hiyo ambayo imeandaliwa na MNH. Watoa mada wengine ni Dk Vicenti Tarimo wa Muhimbili, Dk. Abidan Mganga na Dk. Paul Kissanga.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:03

A 1

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel waje nchini kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya  kilimo.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:01

A

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)  akifungua mkutano   wa wadau wa nishati ulioambatana na uzinduzi wa Jukwaa la Nishati  Tanzania (TEP) kwa niaba ya Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania, Samia Suluhu  jijini Dar es Salaam tarehe 05 Aprili, 2017. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili upatikanaji wa nishati endelevu ya kutosha kwa bei nafuu kwa ajili ya uchumi wa viwanda Tanzania.

Posted On Thursday, 06 April 2017 04:00

A

Mtaalamu wa Nishati kutoka Kampuni ya Argos Energy ya Ufaransa Bw. Laurent Grimaud akiwasilisha mada wakati wa warsha ya siku moja kuhusu nishati mbadala, umuhimu wake na  fursa zinazotokana na nishati mbadala.

Posted On Thursday, 06 April 2017 03:58

AA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mawakala wa pembejeo za kilimo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 5, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na wapili kulia kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvu Tete Ole-Nasha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Posted On Thursday, 06 April 2017 03:57
Page 10 of 1959

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi