We have 268 guests and no members online

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:39

P 1

Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, Daina Matemu, akimuongoza kuelekea kwenye ukumbi wa mahafali, mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (kushoto), wakati wa mahafali hayo, yaliofanyika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Nyuma kulia ni Mwenyekiti Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)  

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:34

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Nilifika kijijini Mkungugu Novemba 2010. Mbali ya kuzunguka na kuongea na baadhi ya wenyeji, moja ya kumbukumbu nilizochukua mahali hapo ni picha ya moja ya nyumba za Mkulima Said Mwamwindi ya tangu mwaka 1971.

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:32

KASSIM-MAJALIWA

Waziri mkuu Kassim Moajaliwa amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kati ya nchi  wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii  zilizopo nchini.

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:31

Ndugu zangu,

Nimekaa sebuleni na Bw. Amani Mwamwindi. Ni nyumbani kwake, Mlandege, Iringa, mwaka 2011.

Amani ni mwana wa Mkulima Saidi Mwamwindi . Amani amepata pia kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa.

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:29

index

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MJUMBE wa Kamati kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Idd ameongoza mamia ya wanachama wa Chama na Wananchi kwa ujumla katika mazishi ya  aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Marehemu Hamdani Haji Machano aliyefariki ghafla jana kwa maradhi ya baridi.

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:28

Picha ya Maggid Mjengwa

Pichani ni picha nyingine ikionyesha nyumba ya aliyekuwa RC wa Iringa Dr Kleruu Inavyoonekana kwa nje.

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:26

Posted On Sunday, 23 April 2017 05:23

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Ni mwaka 2012. Picha ya pamoja na Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Waganga wa jadi mkoa wa Iringa. Hapo yuko Mwenyekiti wao Dr Msekwa Mwenye jacket na kofia. Yuko Dr Mwandulami mwenye batiki. Dr. Kalinga ( Suti nyeusi) Dr. Mkolwa, ndugu yangu Mzee Butinini naye alishiriki kwenye mada na mwingine ni mwandishi Malegesi. Mada kuu ilikuwa Ushirikina. Ni kwenye studio za Ebony FM. Nilisimama kupinga ya ushirikina.
Mambo ya ulozi, kusemasema walisema tumechokaa! Msikilize Sam Mangwana...https://www.youtube.com/watch?v=Fm_hXerLo08

Posted On Saturday, 22 April 2017 05:24

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

KWENYE mazungumzo yangu na Mzee David Butinini mtakumbuka nilimuuliza; Mmoja wa wazee nilioongea nao kwa simu na nilitarajia ningekutana naye kwa mazungumzo ya ana kwa ana ni mkulima Mzee Pesambili . Nilimwuliza Butinini, anadhani Mzee Pesambili angesema nini?

Posted On Saturday, 22 April 2017 05:22

Kushinda lile la Sitti Mtemvu mwaka juzi!

( Kutoka Maktaba ya Mwenyekiti)

Ilikuwa Septemba 3, 1995, Daily News liliripoti, kuwa msichana wa miaka 18, Emily Adolph, pichani, Mwanafunzi wa Central Secondary School, Dodoma, ndiye Miss Tanzania.

Posted On Saturday, 22 April 2017 05:21

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Nimeona wengi mmevutiwa na kumbukumbu hii. Picha za Ikulu Ndogo hii ya zamani ziko kwenye maktaba yangu. Nilizipiga mwaka jana.

Posted On Saturday, 22 April 2017 05:18

GAM1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi.Flora Mazeleng’we alipotembelea uwanja wa Jamhuri Dodoma ili kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano. Aprili 21, 2017.

Posted On Friday, 21 April 2017 17:25

POL

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, leo ameanza ziara ya kutembelea Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kwa kuanzia Ilala.

Ziara yake hiyo itampeleka pia Kigamboni, Temeke, Ubungo na Kinondoni kabla ya kuelekea katika mikoa mingine nchini.

Posted On Friday, 21 April 2017 17:24

madi

Posted On Friday, 21 April 2017 17:22
Page 2 of 1959

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi