We have 151 guests and no members online

Znateli

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo Januari 23.2018, kwenye uzinduzi wa Onesho la Chimbuko la Binadamu Afrika, tukio ambalo litafanyika majira ya saa 11 jioni katika viunga vya Makumbusho ya Taifa, yaliyopo mtaa wa Shabani Robert, mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Posted On Tuesday, 23 January 2018 06:40

Posted On Tuesday, 23 January 2018 06:39

​Muimbaji nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Posted On Tuesday, 23 January 2018 06:36

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Dkt. Otilia Flavian Gowelle akiwa katika mazungumzo na Naibu Balozi wa Israel nchini, Mhe. Michael Baruch Baror kabla ya wawili hao hawajasaini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya Afya kati ya Tanzania na Israel

Posted On Tuesday, 23 January 2018 06:28

. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. 

Posted On Monday, 22 January 2018 06:39

Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . 

Posted On Monday, 22 January 2018 06:33

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw. Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.

Posted On Monday, 22 January 2018 06:31

Benki ya Dunia imetoa ufadhili wa shilingi Bilioni 47 kutekeleza mradi wa uhifadhi wa rasilimali za maji awamu ya pili katika bonde la mto Wami.

Posted On Monday, 22 January 2018 06:29

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama.

Posted On Monday, 22 January 2018 06:13


- Uwanjani 3-1, Vitani Sare

Ndugu zangu,

Kandanda ni zaidi ya mchezo, ni siasa pia. Kuna marais waliobaki madarakani au waliong’oka madarakani kutokana na matokeo mabaya au mazuri ya timu zao za taifa. Soka imeleta uhasama baina ya mtu na mtu, kabila na kabila na hata taifa moja dhidi ya taifa jingine.

Katika historia tunasoma kuwa mchezo huu wa kandanda umewahi kusababisha vita baina ya nchi mbili jirani kule Marekani ya Kusini, ni Honduras na El Salvador.

Ilikuwa ni mwaka 1969 wakati wa mechi za mataifa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1970. Katika mchezo wa kwanza Honduras walikuwa wenyeji.

El Salvador walifika Honduras na wakapata mapokezi baridi sana. Usiku wa kuamkia mechi, wakiwa kwenye hoteli 
waliyofikia, wachezaji wa El Salvador walifanyiwa fujo na wapenzi wa soka wa Honduras waliofika kwa wingi na kuizunguka hoteli yao.
Wakiwa nje ya hoteli waliofikia wageni, wapenzi wale walipiga kelele, waligonga masufuria kwa vyuma na walipiga honi za magari usiku kucha. Masikini, wachezaji wa El Salvador hawakupata nafasi ya kulala usiku mzima. Kulipokucha walionekana kuwa wachovu mno. Walishinda hotelini bila 
kupata nafasi ya kunyosha miguu kwa kutembea mitaani. Polisi waliwaambia wabaki humo humo hotelini kwa usalama wao.

Habari za timu ya taifa kufanyiwa hujuma hizi zilifika nyumbani 
El Salvador hata kabla ya mechi kuanza siku hiyo. Jambo hili liliamsha hisia za utaifa, hasira na chuki kubwa kwa watu wa El Salvador dhidi ya jirani zao Honduras. Muda wa mechi uliwadia. Mechi ilichezwa kwenye uwanja wa Tagucigalpa. Pamoja na vurugu walizofanyiwa na kushindwa kulala usiku, vijana wale wa El Salvador walipigana kishujaa uwanjani kutetea hadhi na 
heshima ya taifa lao. Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kwisha, timu mwenyeji , Honduras walipachika bao la ushindi. Honduras waliibuka washindi kwa bao 1-0.
Nyumbani El Salvador , msichana mmoja aliyekuwa akitazama pambano hilo kupitia luninga alifadhaishwa sana kuona nchi yao ikipoteza mchezo ule katika mazingira yale. Aliamua kujiua.

Kwa moyo wake wa uzalendo na uchungu kwa nchi yake, msichana yule alitajwa kuwa shujaa wa taifa. Mazishi yake 
yalikuwa ya kitaifa. Msafara wa mazishi uliwahusisha pia wachezaji wa timu ya taifa ya El Salvador.

Majuma mawili baadae ikafika siku ya mchezo wa marudiano. Safari hii El Salvador walikuwa wenyeji wa Honduras. Haikuwa mechi ya marudiano ya kawaida, ilikuwa ni mechi ya kulipiza kisasi.

Nini Kilitokea?

Itaendelea kesho.

Maggid.

Posted On Sunday, 21 January 2018 20:51

Image may contain: 4 people, people standing

Image may contain: 2 people, people sitting, table and indoor

 

Ndugu zangu,

Jana mke wangu mpenzi na mimi tulikwenda kuangalia filamu ya The Post. 
Ni mara chache sana mwisho wa filamu unatamani kushangilia kama uko uwanjani kwenye mpira.

Filamu iliyoanza taratibu ilipamba moto katikati na kumalizika kwa kishindo.

Inahusu Vita ya Vietnam na sakata la nyaraka za siri za Pentagon ambazo mwandishi wa The Washington Post alizifanyia kazi. Pamoja na vitisho vya White House, gazeti la Washington Post hatimaye liliweka hadharani ukweli mzima kwa watu wa Marekani.

Pentagon, Idara ya Ulinzi ya Marekani wakati vita vikiendelea ilificha ukweli wa jinsi Marekani ilivyokuwa ikishindwa vita hivyo.

Filamu pia inampa nafasi Mwanamke. Ni pale mwanamama Meryl Streep alivyocheza kwa umahiri mkubwa nafasi ya kuwa mmiliki wa gazeti. Akahimili vitisho na akatoa kauli ya mwisho ya gazeti kuchapwa.

Filamu hii inanikumbusha kisa nilichowahi kuandika hapa juu ya Muhammed Ali na vita vile vya Vietnam mara ile ulimwengu ulipofikiwa na habari za kifo chake. Niliandika..

"Muhammed Ali, Daima Alikataa Kuwa Mbeba Mabuli..

Ndugu zangu,

Usiku wa kuamkia leo ulimwengu umefikiwa na habari za kifo cha mwanamasumbwi mahiri kupata kutokea hapa duniani, ni Muhammad Ali.

Muhammad Ali, atakumbukwa kama shujaa wa wanyonge wa dunia. Alikuwa bondia na mwanaharakati wa haki za wanyonge. Daima Ali hakukubali kuburuzwa.

Hapa nyumbani, Rais Mstaafu , Mzee Ali Hassan Mwinyi amejaliwa kipawa cha kutumia vema lugha ya Kiswahili anapowasilisha ujumbe wake. Kuna wakati alipata kutamka;

“ Ndugu zanguni, kuna wasafiri na wabeba mabuli!”.

Wabeba mabuli ni wale wanaotumiwa safarini kwa kazi ya kubeba hiki na kile, ni kama wapagazi. Wabeba mabuli ni watu wa kuamrishwa safari bila kujua inakwenda wapi. Lakini wabeba mabuli anaowazungumzia Mzee Ali Hassan Mwinyi ni viumbe wenye kufikiri.

Bondia Mohammed Ali alipata kuvuliwa ubingwa wa uzito wa juu duniani kwa kukataa kwenda kupigana vita Vietnam. Alipotakiwa aende vitani Mohammed Ali alikataa na kusema;

“ Siwezi kwenda Vietnam kwa vile sijui hao tunaokwenda kuwapiga wana kosa gani”

Mohammed Ali akaambiwa , kuwa wenzake wameshakwenda huko Vietnam, naye akajibu; 
“ Hao waliokwenda huenda wameshaambiwa kosa walilofanya Wa- Vietnam, miye bado sijalijua”.

Naam. Mohammed Ali hakwenda Vietnam, ni kiumbe aliyefikiri na aliyekataa kuwa mbeba mabuli. Waliompa Mohammed Ali adhabu ya kunyang’anywa mkanda wake wa ubingwa na hata kufungiwa kucheza ngumi kwa muda fulani bado wanamuheshimu Mohammed Ali kwa msimamo wake ule.

Muhammad Ali atakumbukwa daima."

PS: Picha ya juu ni siku Mohammed Ali apotua Dar es Salaam.

Maggid.

Posted On Sunday, 21 January 2018 12:26

Image may contain: 2 people, people playing sports, people standing, grass, outdoor and nature

 

Je, Unaijua Falsafa Ya Kandanda?

Ndugu zangu,

Kandanda, kama dini , ina wafuasi wengi. Mpira ule wa mviringo, wenye kudunda ni kama Mungu wa soka. Bila mpira uwanjani hakuna soka. Kama ulivyo mpira wenyewe, mviringo, wenye sura nyingi na wenye kudunda, basi,hata pambano lenyewe la soka laweza kuwa na sura nyingi. Naam. Mpira 
unadunda, katika soka lolote laweza kutokea.
Soka, kandanda, kabumbu, kipute au ndinga. Yote hayo na mengineyo ni majina yenye kuzungumzia aina moja ya mchezo; mpira wa miguu. Kuna aina nyingi za michezo ya mipira; kuna mpira wa wavu, mikono, meza, pete na 
mingineyo.

Michezo yote hiyo niliyoitaja hapo juu inatofautina sana na mchezo wa mpira wa miguu. Ni kwanini basi michezo hiyo na mingine yenye kuhusisha mpira isiwe na wapenzi wengi kulinganisha na mpira wa miguu? Jibu lake 
linapatikana kwa kutafakari falsafa nzima ya kandanda.

Kandanda huchezwa kwa kutumia miguu. Hii ndio inatufanya wengi tuvutiwe na mchezo huu. Kupitia kandanda tunaona kuwa binadamu anaweza kufanya mambo mengi ya ajabu kwa kutumia mguu wake. Ni mambo yenye kutoa 
burudani kwa anayetazama. Ndio maana hatuchoki kushabikia mchezo huu.

Kama lilivyo jina la mchezo wenyewe, yaani mpira wa miguu, basi, mchezaji haruhusiwi kutumia mikono. Ni golikipa tu anayerusiwa kutumia 
mikono katika kuudaka mpira uliopigwa kwa mguu. Golikipa amepewa eneo lake dogo la kujidai kwa kutumia mikono yake. Nje ya eneo hilo golikipa naye haruhusiwi kutumia mikono, bali miguu.

Mpira unatakiwa wakati wote huwe ndani ya uwanja. Mpira unaotoka nje unaweza kurushwa kwa mikono kuingizwa uwanjani, aliye uwanjani haruhusiwi kuupokea kwa mikono isipokuwa golikipa.

Katika mpira wa miguu mchezaji anaruhusiwa kutumia sehemu 
nyingine zote za mwili, kichwa, kifua, tumbo, mgongo, kisigino na hata kidevu, lakini , kamwe si mkono. Dhambi kubwa katika soka ni kwa mchezaji kuucheza mchezo huo kwa kutumia mkono, na kibaya zaidi akifanya hivyo kwa kudhamiria, kwa makusudi. Dhambi hiyo haisameheki katika soka, adhabu yake 
ni kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mkono ni shetani wa soka.

Waingereza ambao kihistoria ndio waliovumbua mchezo wa soka mwaka 1908, kamwe hawatakoma kumlaani Diego Maradona wa Argentina kwa kufunga goli la mkono nililolielezea hapo juu. Kwa Waingereza, Maradona alifunga goli kwa kumtumia shetani wa soka. Maradona mwenyewe anadai ni mkono wa Mungu!

Mpira wa miguu umechangia katika kuleta furaha kwa mamilioni ya watu hapa ulimwenguni, pale timu ama taifa linaposhinda mashindano muhimu. 
Lakini mchezo huu umekuwa pia ni chanzo cha huzuni kwa mamilioni ya watu katika ulimwengu huu, pale timu au taifa linaposhindwa katika mashindano 
muhimu.

Mpira wa miguu unaingia katika historia ya Dunia kwa kuwa chanzo cha vita baina ya mataifa. Katika mika ya sabini, kule Marekani ya Kusini, 
nchi za El Salvador na Honduras zilingia vitani kutokana namatokeo ya mpira wa miguu baina ya timu za nchi hizo mbili! Mpira ni siasa pia, kuna serikali au viongozi waliobaki ama kuondoka madarakani kutokana na matokeo ya mechi za mpira wa miguu.

Jioni ya leo nitawasimulia kisa kile cha mataifa yaliyoingia vitani kwa matokeo ya uwanjani.

Maggid.

Posted On Sunday, 21 January 2018 12:21

Image result for salum mwalimu

Salum Mwalimu

TAARIFA KWA UMMA, KUHUSU UCHAGUZI MDOGO WA KINONDONI NA SIHA. 

Kamati Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na imefanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018. 

Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo; 

Posted On Friday, 19 January 2018 16:12

Posted On Friday, 19 January 2018 16:11

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amejenga madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo katika kijiji cha Msinune kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Flaviana alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa Msinune mwaka 2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya shule, walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na kumalizia ujenzi wa darasa.

Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa, darasa la saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.

Posted On Friday, 19 January 2018 16:04
Page 11 of 2110

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart