We have 153 guests and no members online

Maji

media

Kimbunga Irmakinatarajia kupiga katika Jamhuri ya Dominika, Haiti na Cuba.

Posted On Wednesday, 06 September 2017 06:52

No automatic alt text available.


...Chagua, Kutaja Wawili Wa Kuchaguliwa, Au Watatu Wa Kuteuliwa...

Zawadi ya mwenyekiti kama kawaida!

Pichani wakipata chai kwenye mapumziko ya kikao cha Bunge Ukumbi wa Kareemjee, enzi hizo.

 
 
Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:19

Image may contain: 5 people, people smiling, people standingNdugu zangu, 

Sisi tuliokua tukiiona bendera ya TANU ikipepea tumeona mengi pia.

Nimesoma kwenye Daily News leo, kuwa Tamasha La Utamaduni Afrika Mashariki linaanza Kampala Alhamisi hii.

Hakika ningependa kuwepo Kampala kushuhudia utamaduni wa A.Mashariki ni upi kwa sasa.

Na hivi, utamaduni ni nini hasa? 
Unahusu mengi, lugha, chakula na hata mavazi.

Nakumbuka utotoni kuna jambo lilinihuzunisha sana wakati nikikua pale Ilala miaka ya 70 katikati.

Kulikuwa na marufuku ya wanawake kuvaa nguo fupi.

Nakumbuka msichana yule aliyekimbilia nyumbani kwetu na kuomba hifadhi asije akachapwa bakora na mgambo wa TANU, kwa vile tu kavaa sketi fupi.

Nakumbuka nilipokuwa nikicheza mtaani na wenzangu nilihuzunika sana kuwaona akina mama wakitembea kwa mashaka. Ilikuwa kawaida kuwaona wanawake wakikimbilia vichochoroni kuwakwepa mgambo wa TANU.

Kama vile waliambizana, wanawake wakaja na mtindo wa kuvaa gauni ndefu maarufu ikiitwa max. Chini kulia gauni la max lilikatwa.
Ilikuwa ni kama protest ya unyanyasaji waliofanyiwa.

Kiukweli gauni la max halikuwapendeza wanawake. Bila shaka, hao hao wanaume waliopiga marufuku ya sketi fupi kuna waliotamani wanawake warejee kwenye kuvaa sketi fupi.

Naam, mitindo hii inakuja na kuondoka, ya miaka ya 70 tunaiona ikirudi tena. 

Si ndio utamaduni wenyewe...!

Zilipendwa...

‘Le Bûcheron’ ... https://www.youtube.com/watch?v=LvDn11AEoas

Picha Ya Maktaba: mjengwablog.com

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:18

Image may contain: 3 people, people standing

 

Niliyaongea Hayo Kwenye Mkutano Na Wanahabari Kuelezea Lengo Na Madhumuni Ya Mdahalo Wa Kujadili Fursa Na Changamoto Za Uwekezaji Kwa Diaspora Na Wajasiriamali Wa Hapa Nyumbani. Ni Ukumbi Wa Makumbusho ya Taifa, April, 12, 2017.
https://www.youtube.com/watch?v=Ha6OWC_ZkzY&feature=youtu.be

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:16

No automatic alt text available."Ni Imani Yangu, Kuwa Huenda Tukawa Wa Mwisho Kuamua Hili Afrika Mashariki, Lakini Itafika Wakati Tutaamua Kama Wenzetu, Halafu, Kama Kawaida Yetu Tutaulizana; Hivi Kwanini Tulichelewa Sana Kuamua?"

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam, 
Sept 5, 2017.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:15

 

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:11

Image may contain: 6 people, people smilingSwali; Ukiwaacha Anna Abdallah ( wa tatu kutoka kushoto), Therezia Makono ( wa nne kutoka kushoto) na Getrude Mongela ( wa kwanza kulia). Wajumbe wanne waliobaki ni akina nani? 
Atakayetaja majina mawili tu na walipo pichani ana zawadi ya mwenyekiti. Na majina yaliyobaki nitawasaidia kujibu.

Maggid

 
 
Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:10

Image may contain: 6 people, people smiling

Image may contain: 1 person, smiling

Image may contain: 1 person, smiling, indoor

 

Ndugu zangu,

Nilitaka nitajiwe majina ya viongozi watatu wanawake wa enzi hizo na walipo pichani.

Inaonekana mara hii swali lilikuwa gumu sana. Hata hivyo, wajumbe wangu wawili; Rosemary Jaha na Mystica Kalunde wamekuwa hodari sana wa kupata jina la tatu, maana wengi mmewatambua Getrude Mongela na Anna Abdallah. Jina la tatu lililotajwa na Rosemary ( Picha ya pili) na Mystica ( Picha ya tatu) kwa wakati mmoja ni Theresia Shija Makono. Ni wa nne pichani kutoka kushoto baada ya Anna Abdallah. Hongera sana Rosemary na Mystica!!

Maggid.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 15:06

Picha hii nimeipiga Mikumi jana jioni.
Maggid,
Dar Es Salaam.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 06:11

Image may contain: outdoor and nature

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:56

Picha no. 1

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimkabidhi zawadi Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka China Sun Long wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari hao iliyofanyika hivi karibuni. Serikali ya China kila baada ya miaka miwili inatuma madaktari wake kwa ajili ya kufanya kazi ya Matibabu ya Moyo katika Taasisi hiyo.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:58

 

Hapo kulikuwa na ajali ya lori na kontena na njia ikafungwa kupisha kulitoa hapo. Magari yote kutoka na kuelekea Iringa yalisimamishwa.
Bahati kwenye kadhia hiyo nilikutana na ndugu yangu na mwanafamilia mwenzangu kwenye media, Assah Mwambene aliyetokea Mbeya kwenda Dar. Tulipata muda mwingi wa kuzungumza.
Maggid,
Dar.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:49

PIX1

Mkurugenzi wa Barabara toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa taasisi hiyo Profesa Godwin Mjema na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:47
Page 12 of 2051

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji