We have 245 guests and no members online

Watumishi

index

Mkutano wa Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho Jumanne tarehe 5 Septemba, 2017 na kumalizika tarehe 15 Septemba 2017 Mjini Dodoma. Shughuli zilizopangwa kufanyika katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:-

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:38

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na baadhi ya Wazee walioshiriki uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 05:08

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea wakati wa kutambulisha shindano la mama msosi linalolaratibiwa na kituo cha radio Nuru FM 93.5 Iringa katika viwanja vya Kata ya Kihesa.

Posted On Tuesday, 05 September 2017 04:59

Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano

Haley amesema teknolojia ya Korea ya Kaskazini kwenye mabomu ya nyukilia ni ya hatari na haina mfano

Posted On Tuesday, 05 September 2017 04:48

media

Rais wa Marekani Donald Trump.

Siku moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la hidrojeni, Rais wa Marekani Donald Trump amelaani vitendo ambavyo ni "vibaya mno na hatari kwa Marekani".

Posted On Monday, 04 September 2017 06:57

index

Na Mahmoud Ahmad Arusha

Chama cha Mpinduzi wilayani hapa kimepokewa wananchama wapya zaidi ya 300 kutoka vyama mbali mbali vya upinzani na kuzindua mashini matatu ya wakereketwa katika kata ya Levolosi jijini hapa.

Posted On Monday, 04 September 2017 06:55

1

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya TEHAMA toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Baltazar Kibola akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuandaa Mipango,Bajeti na kutoa Ripoti  za Malaka ya Serikali za Mitaa utakaozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa  Septemba 5,2017 mjini Dodoma kulia ni Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka mradi wa PS3 Dkt. Gemini  Mtei na kushoto ni Mtaalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago

Posted On Monday, 04 September 2017 06:54

Picha ya Wadhamini TFF, Viongozi wa TFF na wachezaji wa Taifa Stars.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mhe. Mohammed Abdulaziz (wa tatu kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wenzake na viongozi wa TFF mara baada ya chakula cha mchana na wachezaji wa Taifa Starts kwenye Hoteli ya Sea Scape, Kunduchi, Dar es Salaam Septemba 2, 2017. Wengine mstari wa mbele kutoka kushoto ni Ofisi Meneja wa TFF, Bi. Miriam Zayumba, Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Kidao Wilfred, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Abdallah Bulembo; Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Stephen Mashishanga; Rais wa TFF, Bw. Wallace Karia; Makamu Rais wa TFF, Bw. Michael Wambura na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mhe. Balozi Dk. Ramadhani Dau. Taifa Stars baadaye Jumamosi ilicheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kushinda mabao 2-0. (Picha na TFF).

Posted On Monday, 04 September 2017 06:41

 ME1

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipata maelezo mafupi kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuhusu maeneo ambayo miundombinu yake imekuwa kero kwa wananchi,ikiwemo makaravati yaliyoziba na mitaro

Posted On Monday, 04 September 2017 06:50

taifa

Na Mahmoud Ahmad Arusha

Wadau wa masuala ya watoto Pamoja na Serikali wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza sauti za watoto wanazopaza katika kuhakikisha malengo endelevu ya umoja wa mataifa yanafanikiwa ilikuweza kuwasaidia na kufikia malengo yao ikiwemo changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na kuzipatia majibu kwa wakati wakitunga sera.

Posted On Monday, 04 September 2017 06:35


Zawadi ya Mwenyekiti ipo kwa wa kwanza kupata mia kwa mia.
Maggid.

 
 
Posted On Monday, 04 September 2017 06:41

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Image may contain: 3 people, child and outdoor

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting, shoes, child, shorts and outdoor

 

Ndugu zangu,

Naikumbuka vema alasiri ile ya Septemba 2 miaka mitano iliyopita. Jumamosi ile ilionekana ni siku ya kawaida Iringa.

Nakumbuka nilipita Soko Kuu asubuhi ya siku ya tukio. Nilishangaa kumwona kijana aitwaye Majeki akiwa mjini na si Mufindi.

Majeki alikuwa mkereketwa na mpiga debe mahiri wa Chadema.

Majeki akaniambia, huko leo siendi naona hali si nzuri.

Alasiri majira ya saa tisa nikawa na vijana wangu na wenzao kuwafundisha soka kwenye kiwanja cha shule yao. Ni kama inayoonekana kwenye picha ya tatu.

Katikati ya kufundisha soka, ikaita simu yangu. Niliangalia alikuwa Francis Godwin, mwandishi na bloga mashuhuri.

" Mwangosi ameuawa."

Francis hakuwa na maelezo zaidi ya kuniambia ni Mufindi kwenye mkutano wa Chadema.

Nikawajulisha vijana waliokuwa uwanjani kuwa kuna jambo kubwa la huzuni limetokea. Tukatishe mazoezi nifuatilie.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa mara ile nilipopokea taarifa hiyo. Kuanzia hapo nikaanza kuwasiliana na wanafamilia wenzangu wa habari kujua zaidi.

Picha ya pili ni mtoto wa Daudi Mwangosi. Hii ni moja ya picha zenye kunigusa nilizopata kupiga. Mtoto wa marehemu Daud Mwangosi anaonekana akimkumbatia kwa uchungu Dr . Wilbroad Slaa usiku wa Septemba 3, 2013.

Ilikuwa nyumbani kwa marehemu Mwangosi, Mtwivila, Iringa. Nilifika nyumbani hapo usiku huo na kuwakuta watu kadhaa wakiwa kwenye viti nje ya nyumba. Mmojawapo alikuwa Dr Slaa.

Mara akaja mtoto wa kiume wa Daud Mwangosi. Nakumbuka alivyomkubatia Dr Slaa kwa uchungu na kutokwa machozi.

Tuliokaa mahali hapo tulikumbwa na huzuni kuu. Kwenye hali hiyo pichani, anaonekana Mzee Arcado Ntagazwa, Waziri wa zamani kwenye Serikali ya Julius Nyerere.

Jana ilitimu miaka mitano tangu Daud Mwangosi atutoke kwa kuawa kinyama.

Daud ameacha mke na watoto wanne, wa mwisho alikuwa na miaka miwili tu wakati wa kifo chake.

Maggid,

Iringa.

Posted On Monday, 04 September 2017 06:38

PICHA A

Mhashamu Askofu  wa Kanisa  Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu akiongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Posted On Monday, 04 September 2017 06:23

Image may contain: 1 personNdugu zangu, 

Ametutoka, Muhingo Rweyemamu. Kila nilipokutana nae nilizoea kumwita Kaka.

Nilifahamiana na Muhingo kupitia ndugu yangu Absalom Kibanda. Nakumbuka jioni moja mwaka 1996 giza likianza kuingia nyumbani kwetu Kinondoni Biafra , alikuja Absalom Kibanda. 

Nikakaa nae sebuleni. Kibanda akaliweka gazeti la Mwananchi mezani. Kisha akatamka;

" Braza niko na Muhingo tunaomba uanze kutuandikia makala kwenye gazeti hilo tunaloliongoza."

Nilimkubalia Kibanda na hazikupita siku mbili akanikutanisha na Muhingo Rweyemamu pale kwenye ofisi zao, Jengo la CCM Kariakoo.

Muhingo alinichangamkia sana na akaniahidi ushirikiano. Tangu hapo tukaanza kufahamiana zaidi.

Nakumbuka mwaka 2003 nilipata bahati ya kupanda basi moja na Muhingo kuanzia Ubungo kwenda Iringa. Ni basi la Scandinavia. Naweza kabisa kusema, kwenye safari ile ndipo niliweza kumfahamu zaidi Muhingo.

Safari ile ya saa tisa barabarani ilikuwa darasa kubwa na muhimu kwangu. Wakati huo nilikuja likizo nikitokea Sweden. Muhingo aliweza kunieleza mengi anayoyaona na anavyoyatafsiri kupitia uandishi. Muhingo alionyesha kuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya nchi hii hata yale yasioandikwa magazetini.

Mahali fulani kwenye mazungumzo yetu tukaingia kwenye mgogoro wa DR Congo. Muhingo tena akaonyesha alivyo na uelewa mpana wa Nchi za Maziwa Makuu na migogoro yake.

Mathalan, alinisimulia safari yake ya kiuandishi kupitia Rwanda hadi Goma akiwa nyuma ya vikosi vya Laurent Kabila. Alinieleza jinsi askari wale walivyowafuata milimani wanajeshi wa Maimai. Milio ya bunduki na mabomu ilikuwa ni kitu cha kawaida na akazoea. Akanithibitishia pia kuwa askari wa Kagame nao waliokuwepo kwenye operesheni ile ndani ya DRC.

Tukafika Iringa kwa basi kwenye safari niliyoiona fupi sana kutokana na mazungumzo yangu na Muhingo.

Jioni ile nikiwa Iringa, Muhingo aliyekuwa, wakati huo, Mwanafunzi wa Tumaini University, alihakikisha nafika anakoishi pale maeneo ya Semtema. 

Nilipofika Semtema, kwenye nyumba ndogo aliyokuwa akiishi Muhingo, aliishi pia ndugu yangu Assah Mwambene. Naye alikuwa mwanafunzi wa Tumaini University.

Mazungumzo yaliendelea tukiwa watatu kwenye familia ya habari.
Chakula kikapikwa, tukala. Tukaendelea na mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali ikiwamo media na demokrasia. Tuliongea hadi usiku mwingi. 

Kesho yake Muhingo alinialika kutembelea Tumaini University. Nilipofika Chuoni ndipo nilipoona namna Muhingo alivyoheshimika kuanzia kwa wanafunzi wenzake hadi wahadhiri wa chuo.

Muhingo alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji kwenye Serikali ya Wanafunzi. Kwa nafasi yake hiyo alinitembeza kila idara kunionyesha.

Muhingo akaendelea kuwa kaka yangu tuliyeheshimiana na kushirikiana. Kila nilipofika Habari Corporation akiwa Mhariri Mtendaji, Muhingo akioniona naongea na wanafamilia wengine chumba cha habari alikuwa akiniambia;

" Maggid, ukimaliza usiondoke bila kupanda juu ofisini kwangu tuongee."

Akiwa DC Handeni, nilikutana nae pale Chalinze kwenye mgahawa wa Kituo Cha Mafuta cha Kobil. Aliponiona alifurahi sana. Alinitambulisha kwa Mkurugenzi wake wa Halmshauri na kunikaribisha nifike Handeni nikaoene shughuli zinazofanyika huko na kushauri inapowezekana. Alinisisitiza. Bahati mbaya sikuweza kufika Handeni.

Akiwa DC Makete, Muhingo nilikutana nae kwenye Jengo la Akiba ( NSSF) Iringa.

Aliponiona alifurahi sana. Akanitamkia kama alichonitamkia Chalinze. Bahati mbaya tena sikuweza kufika Makete.

Kaka yangu Muhingo umeondoka nikiwa na mengi niliyojifunza kutoka kwako kupitia media. 

Nasikitika pia , sikuweza kukuona na kujifunza kutoka kwako kupitia Utumishi wa Umma kama kiongozi wa Serikali.

Kaka yangu Muhingo Rweyemamu, umeondoka nikiwa na hamu ya siku moja kukaa na wewe tukarejea mazungumzo yetu ya kwenye basi lile la Scandinavia kutoka Dar kwenda Iringa. Kufanya tathmini ya nini kimetokea na nini tafsiri yake.

Nitakukumbuka.

Maggid Mjengwa, 

Iringa.

Posted On Monday, 04 September 2017 05:22
Page 14 of 2051

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart