We have 228 guests and no members online

Znateli

05 62e06

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Picha na OMR

 

Posted On Friday, 29 March 2013 19:54

2 1f1f8

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. Picha na OMR

Posted On Friday, 29 March 2013 19:15

9 1d306

Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu. Picha na OMR

Posted On Friday, 29 March 2013 18:53

1 6eab2

 

Ndugu zangu,

Jana nilimalizia kwa kuandika haya; “miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili; Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.

Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ‘ miwani tofauti’. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa, Oscar na Julius, waliporudi nyumbani?” – Endelea na simulizi hii.

Ndugu zangu,

Hakika, sikufikiri kuwa simulizi hii ingewavutia wengi hivi. Nami nimehamasika kusimulia zaidi. Na hapa ieleweke, kuwa ninapomsoma Mwandishi Stig Holmqvist nalinganisha pia anachokiandika na yale yaliyopatwa kuandikwa na kusimuliwa na wengine. Yale ambayo hata mimi utotoni nimepata kusimuliwa na hata kuyaona. Hivyo, nafanya uchambuzi wa jumla. Msije basi mkashangaa nitakapowarejea waandishi wengine hata yale ambayo mimi mwenyewe nimepata kuyaandika huko nyuma.

Mathalan, wale waliotaka kujua kama kitabu cha Holmqvist kinapatikana kwa lugha ya Kiingereza, jibu lake ni hapana. Lakini, mengine anayosimulia Holmqvist unaweza pia kuyapata kwa lugha ya Kiingereza kwenye vitabu vya waandishi kama   ( The Critical Phase in Tanzania 1945-68:Nyerere and the Emergence of a Socialist Society, Cranford Pratt ) , ( Nyerere of Tanzania, William Edgett Smith) na hata(  The Dark Side Of Nyerere’s Legacy, Ludovick Mwijage) Hiki kimepigwa marufuku.

(Ninanavyo vitabu hivyo na vinginevyo  kwenye maktaba yangu kwa anayetaka kuniazima)

Tuje basi kwenye mwendelezo wa simulizi hii;

Kama inavyoonekana kwenye maandiko ya Stig Holmqvist, kuwa Oscar na Julius waliiona China kwa miwani tofauti.

Julius aliona nini China?

Julius alivyutiwa sana Kiongozi Mkuu Mao. Aliona kuna mengi yanayofanana kati ya China na Tanzania.

Vile Mao alivyowakusanya Wachina kwenye vijiji ilirahisisha kuwafikishia ujumbe kwenye mapambano dhidi ya njaa, umasikini na maradhi. Kwamba ndio njia nzuri ya kuifanya nchi kujitegemea kwa watu wake kushiriki kazi za uzalishazji kijamaa. Lakini pia, kuondokana na sauti zenye kupinga; hivyo kuondokana na upinzani.

Ya China yalifanana sana na fikra za Julius. Na akikumbuka mkutano ule mgumu na Balozi wa Marekani pale Dar, Julius alianza kuiona njia ya kuachana kabisa na Wamarekani. Pamoja na kumwagiwa sifa na John Kennedy alipotembelea White House kwa mara ya kwanza. Julius aliuona ugumu wa kufanya kazi na Wamarekani.

Oscar aliona nini China?

Oscar hakuvutiwa kabisa na Mao. Hakuamini kuwa njia ya Mao ni sahihi pia kufuatwa na Tanzania. Kwenye moja ya kumbukumbu ya ziara yao ya China, kumbukumbu  ambazo Oscar hakupata kuzichapisha, anasema; “ Mao anafanywa kama Mungu. Kutukuzwa kwa Mao hakukumshtua Nyerere, hakuna alichohoji. Mao anakuwa mfano wa kuigwa kwa Nyerere. Na Nyerere anabadili hata staili ya mavazi yake.” ( Oscar Kambona, Pa vag till presidenten, ukurasa wa 200)

Oscar alikubaliana na Julius kuwa Chama kimoja kinaweza kuwa mkakati mzuri  kuzuia mgawanyiko wa kikabila na kimaslahi kama inavyotokea mara nyingi katika nchi za Afrika, na hilo la mwisho walikubaliana lisitokee.

Mara baada ya kurudi kutoka China, haikupita muda, Tanzania ikafanywa kuwa nchi ya Chama kimoja.

Hata hivyo, Oscar na Julius hawakukubaliana juu ya kwa namna gani mamlaka ya uongozi yangegawanywa ndani ya Chama. Na kwa namna gani demokrasia ya mazungungumzo ingeendelezwa ndani ya Chama.

Tangu hapo, dalili za marafiki wawili kuanza kufarakana zikaanza kudhihiri. Na hiki hasa kikawa ni kisa cha marafiki watatu ambacho nilipata kukisimulia kwenye makala zangu za kwenye Raia Mwema. Na marafiki watatu hapa ni  Kambarage ( Julius) Kawawa( Rashid) na Kambona ( Oscar). Na ajabu ya marafiki hawa, wote watatu wana majina ya pili yenye kuanzia na herufi ‘ K’.

Ndio,  wote hawa walikuwa ni viongozi vijana kwenye nchi changa. Walikuwa pia na ushawishi kwenye jamii.

Na ili tufahamu zaidi urafiki wa watatu hawa ni vema tufahamu jinsi walivyokutana;

Nyerere alikutana na Oscar Kambona  wakati Kambona alipokuwa shuleni Tabora mwishoni mwa miaka ya 40. Inasemwa, kuwa Nyerere alimtangulia kiumri  Oscar kwa kupishana miaka mitatu tu. Kule Tabora Nyerere  alikutana pia na Rashid Kawawa, naye alimzidi kiumri kwa miaka mitatu hivi.

Hivyo basi, twaweza kusema, kuwa urafiki wa Julius, Oscar na Rashid ulianzia Tabora, na harakati zao za pamoja za mapambano ya kisiasa zilianzia huko huko Tabora.

Ni nini basi kilifuatia kwenye urafiki wao ? Simulizi hii itaendelea...

Maggid Mjengwa,                       

Iringa.

0788 111 765

http://mjengwablog.co.tz

Posted On Friday, 29 March 2013 09:45

308207 10151505185183058 749260888 n 84a87

ajali-ghorofa 00766

Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde kuwa kuna ghorofa limeanguka eneo la kariakoo jijini Dar es salaam , Habari zaidi zitakujia

Updates

Takriban watu watatu wamethibitishwa kufariki baada ya jengo lenye ghorofa zaidi ya kumi kuporomoka mjini Dar es Salaam, Tanzania.Waokozi wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta na kuwaokoa manusura na wanasema kuwa hadi sasa watu kumi na watatu waliokuwa wamenaswa wameokolewa.


Zaidi ya wengine arobaini wangali wamenaswa chini ya vifusi.Shughuli ya ujenzi ilikuwa inaendelea kwenye jengo hilo wakati lilipoporomoka katikati mwa mji wa Dar es Salaam.Miongoni mwa watu ambao wangali kupatikana ni wafanyakazi wa mjengo na watoto kutoka shule jirani ya mafunzo ya dini ya kiisilamu.Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada."nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia mayowe,'' alisema shahidi mmoja.Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na liliporomoka saa tatu kasorobo asubuhi kwa saa za Afrika mashariki.Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado haujulikani.

Posted On Friday, 29 March 2013 08:16

2 f23d9

Ni kwa wagonjwa na watoto yatima Arusha. Pichani ni Mwenyekiti wa Mfuko huo Mheshimiwa Catherine Magige.

Posted On Thursday, 28 March 2013 21:02

9 57afd

Ndugu zangu,

Na ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza; `` E nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.”

Nao wakamwuliza; ``Tukaandae wapi?''

Yesu akawajibu; ``Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni huyo huyo, mpaka kwenye nyumba atakayoingia.”

“Kisha mwambieni mwenye nyumba; Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani. Chumba kilicho na fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.''

Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka. Wakati ulipofika, Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia;

``Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.''

Hapo Yesu akapokea kikombe cha divai, akashukuru akisema, ``Chukueni mnywe wote. Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.'' Alitamka Yesu.

Ni Neno La Leo.

Nawatakia nyote Pasaka Njema!
Maggid,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz

Posted On Thursday, 28 March 2013 20:49

8 7968f

Ndugu zangu,

Nikiwa Mbeya, alasiri moja, Oktoba 1989 niliipiga picha hii pale Soko Matola. Ulikuwa ni wakati wa vuguvugu la mabadiliko ya upepo wa kisiasa duniani. Ni baada ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.

Na hapa nyumbani yalianza pia kuchomoza magazeti huru. Nakumbuka siku hiyo lilifika Mbeya gazeti liitwalo ' Motomoto'. Liligombewa sana, maana, lilikuwa na habari ' motomoto' haswa, si za ' uvuguuvugu!'

Leo hii vichwa vile vya habari vya kwenye ' Motomoto' visingewashtua wasomaji, mathalan; " Waziri awekwa kitimoto!" Ni mambo ya kawaida sana kwa sasa.

Naam, tumetoka mbali!
Maggid ,
Iringa.
http://mjengwablog.co.tz/

Posted On Thursday, 28 March 2013 19:57

6 305b6

Picha ya Mtandaoni.

Posted On Thursday, 28 March 2013 19:29

3 2ec40

Posted On Thursday, 28 March 2013 19:11

 

2 400e53 e4b21

3 e4b21

Posted On Thursday, 28 March 2013 05:37

1 49656

Ndugu zangu,

Niliandika juzi, kuwa mwaka 1964  yawezekana kabisa ndio ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa Julius Nyerere katika kipindi chake chote cha Uongozi wa nchi hii.Ni mwaka uliokuwa na matukio makubwa yaliyoitikisa nchi na Rais mwenyewe. Kulikuwa na Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12. Kukawa pia na uasi wa jeshi wa Januari 20, na matukio mengine yakafuatia.
 
Mwandishi Stig Holmqvist kwenye kitabu chake; Pa vag till presidenten – ‘ Njiani kwenda kwa Rais’,  anaulezea mkutano mgumu kati ya Julius Nyerere na Balozi wa Marekani Tanzania, Leonhart.Julius Nyerere alikwenda mwenyewe kwa Balozi kufafanua kilichotokea na kupelekea kuridhia Balozi mdogo wa Marekani Unguja  afukuzwe nchini.
Ujumbe wa siri kwa njia ya telegramu kutoka kwa Balozi Leonhart kwenda White House na CIA unabainisha jambo hilo.Inaelezwa na Balozi huyo, kuwa siku hiyo ya mkutano wake na Julius, Januari 16, 1964, kuwa  hali haikuwa nzuri.

Balozi Leonhart anasema; “ ....Nyerere alitingisha kichwa na hakutaka hata kuniangalia....”Tumeona, kuwa katika mkutano ule, Julius Nyerere, pamoja na kutambua mapungufu, lakini alikataa katakata kubadili msimamo wake wa kumfukuza balozi huyo mdogo wa Marekani.Julius alikuwa na miaka mitatu tu kama Rais. Alikuwa kijana wa miaka 42 tu. Na Chama chake cha TANU kilikuwa  hakijatimiza hata miaka kumi. Na yeye mwenyewe, Julius, kumbukumbu za kutumia  chaki za ubaoni kama mwalimu wa pale Pugu Sekondari huenda zilikuwa bado hazijamtoka. Lakini, pale kwa Balozi wa Marekani, alikaa na kuongea kama Rais wa Tanzania. Ndio, alikuwa Rais mchanga kwenye nchi changa. Julius hakuwa na uzoefu wa siasa za kimataifa na hasa inapohusu ‘ michezo ya wakubwa’- Marekani na Uingereza kwenye upande mmoja, na Soviet Union, China na Cuba kwenye upande wa pili.

Yawezekana pale Ubalozini Julius alikumbuka usemi wa wahenga; “ Kua uyaone!”Ikumbukwe,  Julius alimfanya rafiki yake wa karibu, Oscar Kambona kuwa Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje. Na Oscar naye hakuwa na uzoefu. Hivyo, wote wawili; Julius na Oscar.Miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili;  Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ‘ miwani tofauti’. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa,  Oscar na Julius,  waliporudi nyumbani?

Panapo majaliwa nitawasimulia...

Pasaka Njema.
Maggid,
Dar es Salaam
http://mjengwa.co.tz

Posted On Thursday, 28 March 2013 01:43

1 9b822

Kona ya Jamhuri na Morogoro Road, Dar.

Posted On Thursday, 28 March 2013 00:51

6 805ee


Leo kwa mara ya kwanza nimetafakari kitu ambacho sijawahi kukifanya kwa miaka mingi; kuwapangisha wageni wangu kwenye Hotel ya kiwango cha Kimataifa na ya gharama nafuu mno, lakini iko Kariakoo.

Ni mara yangu ya kwanza kutembea kwa miguu jioni nikiwa na wageni wangu kutoka maeneo ya Posta na kuvuka Bustani ya Mnazi Mmoja kwenda walikofikia wageni wangu Kariakoo.

Naamini kabisa, kuwa kama mitaa zaidi ya Kariakoo itawekwa lami na taa za barabarani, basi, Kariakoo itakuja kuwa ni mahali ambapo hata wenyeji wa Dar watapenda kutembelea nyakati za usiku.
Pichani ni mgeni wangu akiwa kwenye moja ya hotel za kisasa na za gharama nafuu ndani ya Kariakoo.

Posted On Wednesday, 27 March 2013 19:55

3 45996

 Hapa niliwapeleka wageni wangu usiku huu. Wamenjoy sana! Kulikuwa na muziki wa rhumba kuanzia Kwasakwasa hadi Ndombolo ya Solo, ' live' kutoka kwa Dj wa Capital Radio.
Kariakoo ya siku hizi si kama ile ya zamani!

Posted On Wednesday, 27 March 2013 19:46

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi