We have 279 guests and no members online

SAN1

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Chama cha Ngoma  na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao Ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngoma na Muziki Asili Tanzania Leo April 21, 2017.

Posted On Friday, 21 April 2017 17:20

tanzania

Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo  watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale  wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya.

Posted On Friday, 21 April 2017 17:18

MW2

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.

Posted On Friday, 21 April 2017 17:13

unnamed

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu.

Posted On Friday, 21 April 2017 04:45

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

UKIMWONA kwenye mitaa ya Iringa bado anatembea kwa hatua za kijeshi. Ni David Butinini ( Pichani kulia).

David Butinini ni kachero mstaafu wa jeshi la polisi . Butinini alishuhudia kwa macho yake, siku Mkulima Said Mwamwindi alipofika kituo cha Polisi Iringa akiwa na mwili wa marehemu Dk. Kleruu kwenye gari aliloendesha.

Posted On Friday, 21 April 2017 04:41

media

Bunge laUingereza limeunga mkono hoja ya Waziri Mkuu Theresa May ya kufanya uchaguzi wa mapema

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:31

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:30

Picha ya Maggid Mjengwa

Alikuwepo kupaza sauti za diaspora kwenye Tanzania Diaspora Easter Investment Forum 2017. Dr Hamza Mokiwa alimwakilisha mwenyekiti wa TDC-Global, Ndugu Abraham Sangiwa.

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:29

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimpima Mama Mjamzito moyo wa mtoto aliyepo tumboni ili kuangalia kama una magonjwa au la. Mwishoni kwa mwaka jana Taasisi hiyo iliwapima wajawazito 25 kati ya hao watano watoto wao walikutwa na matatizo ya Moyo.Picha na Anna Nkinda – JKCI.

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:27

Picha ya Maggid Mjengwa

Pichani ni kwenye mdahalo kujadili fursa na changamoto za kufanya biashara na uwekezaji nchini kwa kuangazia mchango wa diaspora na wajasiliamali wa nyumbani. ( Tanzania Diaspora Easter Investment Forum 2017). Kutoka kulia ni Ndugu Godwin Kidulile, mkulima na mjasiliamali, Edith Chenga Chamvi, mtaalamu wa masuala ya kijamii kutoka Denmark, George Fumbuka, mtaalamu wa masuala ya uchumi aliyebobea kwenye masuala ya mauzo na manunuzi ya hisa, Jennifer Bash, mwenyekiti mwenza wa mdahalo, na mimi.

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:25

Na Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

Posted On Thursday, 20 April 2017 04:23
Page 3 of 1959

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi