We have 169 guests and no members online

Maji

kp07032013 64ef4

Posted On Friday, 08 March 2013 02:46

IMG_3758  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. wa pili kulia  ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho kulia ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 7.3.2013.(PICHA NA JOHN LUKUWI)

Posted On Friday, 08 March 2013 02:42

 

DSCF0014Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Ngosi Mwihava akisoma hotuba ya ufunguzi katika warsha ya mabadiliko ya tabia nchi inayoendelea mjini Bagamoyo jana PICHA NA EVELYN MKOKOI

Posted On Friday, 08 March 2013 02:37

 

 Mwanvita Makamba, akiwa katika Chumba alicholazwa Mhariri Mkuu Mtendaji, wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalom Kibanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, wakati alipomtembelea kumjulia hali katika Hospitali ya Milpark baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo jana usiku nchini Afrika ya Kusini. Picha na Amani Tanzania

Posted On Friday, 08 March 2013 02:33

d (1)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Hell Thorning-Shmidt  katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu jana usiku

Posted On Thursday, 07 March 2013 20:16

Photo: ... Na Msaidizi Wa Mwenyekiti Naye Alitekwa Na Majambazi Jana Usiku!
Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"
Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.
Masikini, akafikwa na balaa la kutekwa na majambazi kwenye bajaji.  Nilikofikia Dar nikaamshwa saa kumi za usiku. Mlinzi akaniambia kuna ndugu yako amekuja na teksi hata nguo hana. Amebaki na nguo ya ndani tu. Amekabwa na majambazi.
Nikamsaidia Ludovik. Na kwa vile yeye ni Yanga, basi, nikahakikisha nampa suruali na jezi ya Simba!
Naam, iko siku, kila mtu ataishabikia Simba!
Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo.

Pichani Ludovick akisimulia mkasa uliomkuta kwa Mwanzo Millinga na Joseph Kulangwa. Ndugu yangu Kulangwa ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Habari Leo.

Kijana Ludovik Joseph. Tulikula wote na kuongea pale Rose Garden jana usiku. Tuliondoka kwenye saa tano usiku. Nikamfikisha mpaka kona ya Shekilango na Morogoro Road. Hapo aliniambia angepata daladala öa kumfikisha nyumbani kwake. Nilimwuliza jambo tu; " Ni salama hapa kukuacha?"
Akanijibu ni salama maana amesafiri mara kadhaa katika muda huo.

Posted On Thursday, 07 March 2013 17:40

Wazazi wa aliyekuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)marehemu Benson Mollel,Suzana na Peter Mollel wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu mtoto wao jana nyumbani kwao Lemara jijini Arusha.Picha na Moses Mashallah 

Posted On Thursday, 07 March 2013 17:03

 Wakala wahuduma za mtandao wa  Vodacom Tanzania, KilibeJumbe,akimuelimisha mkazi wa Kongowe, Dar es Salaam, namna atakavyonufaika baada ya kutumia vifurushi vilivyopo katika mtandao huo, kufuatia kampuni hiyo hivi karibuni kufunga minara ya 3G kuzunguka maeneo yote ya Dar es Salaam, minara hiyo inatoa fursa kwa mteja wa Vodacom kupiga simu na kupata huduma bora za intanet.

Posted On Thursday, 07 March 2013 16:07

 

02Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Posted On Thursday, 07 March 2013 15:04

 

Picha na 1     

    Na. Aron Msigwa – MAELEZO. 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wanawake nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za maendeleo zinazojitokeza katika maeneo yao ili waweze kujikwamua kiuchumi na kupambana na umaskini. Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika machi 7 mwaka huu. Amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwezesha upimaji wa utekelezaji wa maazimio , matamko, mikataba na itifiki mbalimbali za kimataifa na kikanda zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia kwa wanawake na kubainisha kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo Uelewa wa Masuala ya Jinsia katika Jamii; Ongeza kasi“ Amesema serikali ya

Posted On Thursday, 07 March 2013 14:55

 

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefungua Mkutano wa pili wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) jijini Dar es Salaam na kuzindua uuzwaji wa Nyumba za mradi wa Mfuko huo pamoja na Uchangiaji wa hiyari kwa Watu wasio watumishi wa Umma. Pichani Meza kuu kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Katibu Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini PSPF, George Yambesi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.

Posted On Thursday, 07 March 2013 14:48

Mama mjasiliamali akiuza Nyanya njeyasokola mashinetatu mjini Iringa bei kwasasa ni Sh 2500 kwa ujazo wa kipimocha lita 4 36101

Posted On Thursday, 07 March 2013 14:39

 

IMG_1202

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkuu wa Utumishi wa MCC Bw.Steve Kaufmann,akiongoza ujumbe wa viongozi wa MCC waliofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Posted On Thursday, 07 March 2013 10:01

 

2005-02-07 04.12.59

Mkrugenzi wa shirika la NGOs akiwaeleza wajumbe namna shirika lake linavyofanya kazi  katika ziara ya wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Uratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali walipotembelea shughuli za NGOs Mkoani mwanza mara baada ya kufanya kikao.

Posted On Thursday, 07 March 2013 09:46

IMG 9450 54548

Picha na Mbeya yetu blog

Posted On Thursday, 07 March 2013 09:24

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji