We have 162 guests and no members online

Simu

bajaji1 1940c

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mh Edward Lowassa amekabidhi pikipiki  nne za miguu mitatu maarufu kama majaji za kubebea mizigo  zenye thamani ya kiasi cha  shilingi millioni 50 kwa umoja wa vijana wilaya ya Monduli, ili kusaidia vijana kukabiliana na tatizo la Ajira.Pichani Mh Lowassa akikabidhi pikipiki hizo kwa mmoja wa viongozi wa matawi ya vijana wilayani hapo, yumbani kwake Ngarash Monduli.

Posted On Tuesday, 19 February 2013 09:50

Photo: Matokeo ya Form Four ni kioja kingine!
Ndugu zangu,
Jioni yote hii nilikuwa nimepumzika kujisomea tu, hata taarifa ya habari imenipita. Muda huu nilipoingia mtandaoni nakutana na habari hii ya kusikitisha; matokeo mabaya ya kidato cha nne!
Namkumbuka jamaa yangu aliyeniuliza; " Maggid, unatarajia nini pale unapoona mwalimu anahonga ili apewe nafasi ya kwenda kusahihisha mitihani?" Kioja hiki!
Nakumbuka pia miaka kadhaa iliyopita. Mzazi kule Musoma alikwenda kulalamika kwa Mwalimu Mkuu aliposikia mtoto wake amefaulu mtihani wa darasa la saba na amechaguliwa kujiunga na Sekondari. Mzazi yule akauliza kwa kushangaa; " Hivi aliyefaulu ni mtoto wangu huyu huyu ambaye mpaka hii leo hajui vema kusoma na kuandika?"- Kioja!
Na nimeona, kwenye matokeo yaliyotoka hii leo, kuwa kwenye shule iliyopewa jina la  Sekondari ya J. M. Kikwete  wanafunzi wote wamefeli! Kioja hiki!
Tunajifunza nini?
Tuna MGOGORO WA ELIMU- Education Crisis. Ni mgogoro wa kitaifa. Tuna lazima ya kutafuta suluhu ya pamoja kama taifa.  Hapa si mahala pa kutanguliza siasa za vyama. Inahusu taifa letu na mustakabali wake.
Hivi tunajua? Kuwa umejengeka mfumo sasa wenye kuashiria kuwa kuna ' Ubaguzi wa Kielimu'. Kwamba matokeo haya mabaya ya Form Four yanawahusu zaidi watoto wa makabwela na kwenye shule za makabwela.
Ni matokeo ya Serikali kutowekeza rasilimali nyingi kwenye shule za Msingi na Sekondari za umma ( Public Schools). Hii ni pamoja na kuhakikisha walimu kwenye shule hizo wanapata mafunzo yenye ubora vyuoni, na pia wanapata mishahara na marupurupu ya kuwafanya wajivunie kuwa walimu kwenye shule za umma- public schools.
Kuna tunaokumbuka, kuwa enzi zile, sisi tuliosoma kwenye Sekondari za Serikali, ndio tulioonekana kupata bahati ya kwenda kwenye shule zilizo bora kuliko zile za binafsi. Ni kwa sababu, mfumo wetu wa elimu haukuwa wa kibaguzi. Kwamba darasa la shule ya msingi niliyosoma mimi pale Kinondoni , alisoma pia mtoto wa Waziri wa Maji, Gwassa Sebabili.
Sekondari ya Tambaza niliyosoma mimi alisoma pia mtoto wa Mzee Ali Hassan Mwinyi, huyu huyu Dr. Hussein Mwinyi. Hivyo, Baraza la Mawaziri lilipokutana na kuzungumzia matatizo ya elimu, kimsingi walizungumzia matatizo ya elimu ya watoto wao katika shule ambazo watoto wao wamechanganyika na watoto wa makabwela.
Leo hii kama kwenye Baraza la Mawaziri atatokea Waziri atakayezungumzia matatizo ya shule ya Sekondari ya Kata anayesoma mwanawe pale Makumbusho, basi, kuna wenzake watakaomwangalia kwa mshangao, na kujiuliza pia; " Hivi huyu Mheshimiwa ameshindwa kumpeleka mwanawe hata pale Sekondari ya Saint nanihii!"
Naam, tunachokiona sasa ni kichuguu cha tatizo, mlima wenyewe hatujaufikia.  
NI JIONI YA KUSIKITISHA SANA. ( Picha hiyo juu niliipiga shule ya msingi Ikuvala, Kilolo, Iringa, miaka kadhaa iliyopita)
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765


Ndugu zangu,
Jioni yote ya jana nilikuwa nimepumzika kujisomea tu, hata taarifa ya habari ilinipita.Nilipoingia mtandaoni nikakutana na habari hii ya kusikitisha; matokeo mabaya ya kidato cha nne!

Namkumbuka jamaa yangu aliyeniuliza; " Maggid, unatarajia nini pale unapoona mwalimu anahonga ili apewe nafasi ya kwenda kusahihisha mitihani?" Kioja hiki!

Nakumbuka pia miaka kadhaa iliyopita. Mzazi kule Musoma alikwenda kulalamika kwa Mwalimu Mkuu aliposikia mtoto wake amefaulu mtihani wa darasa la saba na amechaguliwa kujiunga na Sekondari. Mzazi yule akauliza kwa kushangaa; " Hivi aliyefaulu ni mtoto wangu huyu huyu ambaye mpaka hii leo hajui vema kusoma na kuandika?"- Kioja!

Posted On Tuesday, 19 February 2013 09:27

sikika cd3b2

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

18 Februari, 2013

Sikika yampongeza Waziri Mwinyi kwa Kuwajibika

Sikika inapenda kumpongeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi kwa
kuweka bayana na kukiri kwamba kuna uhaba mkubwa wa dawa muhimu za kutibu malaria,
maarufu kama dawa mseto (Alu) katika vituo vingi vya huduma za afya vya umma nchini.

Posted On Tuesday, 19 February 2013 09:08

Photo: Neno La Leo: Ya Padri Mushi Na  Ugumu Usiokuwepo Wa Kurudi Misri!
Ndugu zangu,
Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.
Bado, kama taifa, tuko kwenye  mshtuko wa kuawa kwa Padri Mushi kule Unguja. Swali bado linaning'inia vichwani; KWANINI?
Watanzania kwa asili ni ndugu, haya ya tofauti za kidini hayajawahi kuwa tatizo kwetu. Mathalan, asubuhi hii nilikuwa naongea na ndugu yangu kijijini Mahango, Madibira, Mbeya. Anaitwa Salim Mjengwa, yeye ni Muislamu, baba yake, Raphael Mjengwa ni Mkristo. Na kwenye familia yao wamechanganyika Waislamu na Wakristo. Kamwe haijawa tatizo kwao wala kwa sisi ndugu zao.
Jana jioni niliongea na Padri Manfred Mjengwa, naye ni mdogo wangu. Alikuwa njiani kwenda msibani Unguja kumzika Padri mwenzake na rafiki yake waliofanya kazi pamoja alipokuwa Zanzibar. Ni Padri Mushi. Ukristo wa Manfred sijapata kuuona ni tatizo kwenye ukoo wetu uliochanganyika kiimani. Hata mmoja wa watoto wangu nimempa jina la baba yake mdogo, anaitwa Manfred. 
 Ndugu zangu,
Kuna tulikotoka na tumeanza kupasahau. Nimepata kuandika yafuatayo, kuwa ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri. Hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna Wana wa Israel wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. 
Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.
 Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi  iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.
 Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ‘ Wao Wakristo’ na ‘ Sisi Waislamu’. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ‘ Nchi Yetu’ na maslahi yake.
Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.
Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).
 Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.
 Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.
Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.
 Kuna hata wenye kufikia kutamka; ‘Nchi hii ina wenyewe’. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.
Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.
 Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.
Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya ‘kila mtu na lwake’. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.
 Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.
 Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
 Iringa,
0788 111 765, 0754 678 252
<a href=


Ndugu zangu,

Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Bado, kama taifa, tuko kwenye mshtuko wa kuawa kwa Padri Mushi kule Unguja. Swali bado linaning'inia vichwani; KWANINI?

Posted On Tuesday, 19 February 2013 08:54

MSIBA WA MOTO 2 879d6

Na John Banda, Dodoma

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nzuguni iliyopo manispaa ya Dodoma amekufa kwa kujichoma moto baada ya Mjomba wake kumchapa viboko kutokana na kosa la kutomsaidia Bibi yake kuosha vyombo.

Tukio la kifo cha mwanafunzi huyo lilitokea jana jumapili ambapo saa 11 jioni katika hospital Rufaa ya General Dodoma baada ya kulazwa kwa masaa kadhaa

Posted On Tuesday, 19 February 2013 08:24

240x_mg_162684_595768906_415200831853pm3098504Likiwa limetokea kwenye wiki la mafanikio makubwa katika majijini ya Johannesburg nchini Africa ya Kusini na Tunis, Tunisia ambako iyalifanyika mapambano mawili ya ubingwa wa dunia kwa vijana na ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ambako Illunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) aliukwea ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Cruserweight baada ya kumsambaratisha Gogito Gorgizadze kutoka nchini Georgia. Aidha bondia Ayolub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium kumkata ulimi bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana,  Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa)  linajiandaa tena kwa mapambvano mawili makubwa mwezi ujao.

 

Posted On Tuesday, 19 February 2013 08:03

imagesDeutsche Welle inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili
chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu
itakayofanyika jijini Dar es Salaam
Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari

za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya
Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu. Tarehe 22 Februari, saa
9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea
maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwa-
leta pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya
“ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.

Posted On Tuesday, 19 February 2013 07:44

tff_LOGO1KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na Idd Mtiginjola imetupa maombi ya kufanyia marejeo (review) uamuzi wake kama yalivyowasilishwa mbele yake na waombaji watano.

 

Posted On Tuesday, 19 February 2013 07:31

FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao

kilichotokea jana asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam
alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

 

Posted On Tuesday, 19 February 2013 07:24

g 002 e1b2e

Posted On Tuesday, 19 February 2013 06:14

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II (wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki askofu Dimistrious

Posted On Tuesday, 19 February 2013 04:15

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (Pichani) amewataka wakatoliki na watanzania kwa jumla kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo kumetokea kundi la watu wachache kutaka kuvunja amani  hapa nchini kwa kutumia udini.

 

Posted On Tuesday, 19 February 2013 03:41

Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka

 

Posted On Monday, 18 February 2013 20:20

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE) ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012

 1.0UTANGULIZI

 Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :

 2.0MTIHANI WA MAARIFA (QT)

2.1Usajili na Mahudhurio

 Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176

 Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani. 

Posted On Monday, 18 February 2013 16:47

 

 

tff_LOGO1

                                   SIMBA YAINGIZA MIL 134/-, AZAM MIL 34/-

PAMBANO la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Libolo FC ya Angola lililofanyika jana (Februari 17 mwaka huu) limeingiza sh. 133,795,000 wakati lile la Kombe la Shirikisho kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini lililochezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) limeingiza sh. 34,046,000. Watazamaji 22,469 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Simba kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Simba ilipoteza pambano hilo kwa bao 1-0. Mgawo wa mechi hiyo

Posted On Monday, 18 February 2013 15:09

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji