We have 160 guests and no members online

Maji

.

Posted On Saturday, 16 February 2013 06:39

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.

Posted On Saturday, 16 February 2013 06:01

5

Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo  mkabala na Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal Dk.Eliezer Feleshi, Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh Ponda aachiwe huru.

 

Posted On Saturday, 16 February 2013 05:35

1.

Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya.

 

Posted On Friday, 15 February 2013 21:46

8E9U0677

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakishiriki ibada ya Mazishi ya Askofu Dkt.Thomas Laizer iliyofanyika katika kanisa na Usharika wa mjini Kati.mjini Arusha leo.

(PICHA NA IKULU)

 

Posted On Friday, 15 February 2013 21:40

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)
anaeshughulikia masuala ya Siasa, Dk. Julius Rotich (wapili kushoto)
akizungumza leo katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu
ya zoezi la Uteketezaji wa Silaha ndogo ndogo litakalo fanyika Ukonga chini ya
usimamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania. Pamoja nae kutoka kushoto ni Mtaalam

 

Posted On Friday, 15 February 2013 21:36

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la ushauri la watumiaji wa nishati na maji nchini na wadau wake walipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za baraza hilo. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pongezi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuahidi kuwachukulia hatua walanguzi wa nishati ya mafuta pamoja na wale wanasimamia kwa kushindwa kufanya kazi yao vizuri. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.

 

Posted On Friday, 15 February 2013 15:57

2-mazumgumzo sho Waziri na sally cac26

Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenella Mukangara (Mb)akizungumza na Mkurugenzi wa British Council nchini(kulia) Sally Robinson leo alipomtembelea Ofisis kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya tasnia ya Utamaduni.

Posted On Friday, 15 February 2013 13:26

  Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kushoto) akiwakabidhi bati 24 kwa viongozi wa CCM Tawi la Kwa Mayambi, kata ya Sungaji ili kuezekea jengo la Ofisi.

Posted On Friday, 15 February 2013 12:26

Christine Mhando 7315c

Na Freddy Macha

Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake
cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu
leo Ijumaa mjini London.

Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya
Kiswahili). Yametayarishwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania London na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani.

Posted On Friday, 15 February 2013 11:56

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akimsalimia Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta (Kulia) wakati alipokuwa anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Edema mjini Morogoro kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya Jinsia kwa maafisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.

Posted On Friday, 15 February 2013 11:48

 

UG CJ 1Jaji Mkuu wa Uganda Mhe. Benjamin Odoki (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana (alhamisi Feb. 14 2013) kuhusu uzoefu wake katika uandishi na utekelezaji wa Katiba. Jaji Odoki aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.

UG CJ 2

Jaji Mkuu wa Uganda Mhe. Benjamin Odoki (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Jaji Odoki, ambaye aliongoza Tume ya Katiba ya Uganda iliyoundwa mwaka 1989, amekutana na Wajumbe wa Tume jana (alhamisi Feb. 14, 2013) na kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya.

Posted On Friday, 15 February 2013 10:17

Na: Frederick Katulanda, Mwanza- Mwananchi

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti. Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza. Baada ya kunaswa kwa mtuhumiwa huyo,

Posted On Friday, 15 February 2013 09:46

Photo: " Nyama nyama nyama!.... Nyama!... Nyama ya farasi....?
Je, unakumbuka mchezo huu wa utotoni tulipojifunza ipi nyama na ipi si nyama?
... Nasikia huko Ulaya madukani wanauza nyama ya farasi. Makubwa hayo!
Pichani ni Hoyce Temu kwenye shamba la mifugo la Salim' Asas' Abri, Isimani, Iringa, hivi karibuni.


Je, unakumbuka mchezo huu wa utotoni tulipojifunza ipi nyama na ipi si nyama?

... Nasikia huko Ulaya madukani wanauza nyama ya farasi. Makubwa hayo!

Pichani ni Hoyce Temu kwenye shamba la mifugo la Salim' Asas' Abri, Isimani, Iringa, hivi karibuni.

 

 

Posted On Friday, 15 February 2013 09:26

 

_DSC0321

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sazi Salula akifungua Warsha ya Maafisa Mazingira wa Majiji  kuhusu kukuza uelewa wa kuandaa taarifa ya Hali ya Mazingira   kwa  Majiji ya Mwanza,Arusha, Mbeya na Tanga. Warsha hiyo iliyofanyika Giraffe Hotel, Dar es Salaam

_DSC0329

Baadhi ya Maafisa Mazingira wa Majiji Wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais[pichani hayupo] alipokua anafungua Warsha ya Majiji kuhusu Kukuza Uelewa wa Kuandaa Tarifa ya Hali ya Mazingira ya Majiji iliiofanyika kwenye Hotel ya Giraffe Jijini Dar es Salaam.

Posted On Friday, 15 February 2013 09:35

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji