We have 161 guests and no members online

Simu

 

ndc

Dk Anacleti Kashuliza Katibu Mtendaji wa  Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  NCC akibadilishana mikataba wa ushirikiano kuwawezesha wananchi na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Bw. Shannel Mvungi           

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wameanzisha ushirikiano utakaowawezesha wananchi kiuchumi katika maeneo ambayo NDC imeanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo. Manufaa haya kwa wananchi yanatokana na kusainiwa kwa Makubaliano ya ushirikiano kati ya mashirika haya ambao unalenga kutoa fursa kubwa za ushiriki wa kiuchumi kwa wananchi wa maeneo husika.Hadi sasa,

Posted On Friday, 15 February 2013 09:19

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu: Ukimya Wa Marafiki Unaumiza Zaidi Kuliko Kelele Za Maadui...!
Ndugu zangu, 
Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na  Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.
Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.
Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 
Nilikuwa na miaka 12 tu. Nakumbuka niliisikiliza hotuba ile kutoka mwanzo hadi mwisho; neno kwa neno.  Nikiri, kuwa Julius Nyerere alikuwa hodari sana kwenye rhetoric- sanaa ya kuzungumza.
Kwa mtawala, kuamrisha vikosi vya nchi yako kwenda vitani ni moja ya maamuzi magumu sana. Na wakati mwingine, hotuba ya kuamrisha vita yaweza kuamua hatma ya vita. 
Kwenye hotuba ile, Julius Nyerere  aliweka vema msingi wa hoja, ya kwanini, sisi , kama taifa, tulilazimika kwenda vitani.
Na akatamka yafuatayo yaliyosisimua na kuhamasisha vikosi na taifa kwa ujumla. Kwamba;
- Uwezo wa kumpiga Amin tunao...
- Sababu ya kumpiga Amin tunayo..
- Na nia ya kumpiga Amin tunayo...
Kisha akatoka nje ya mipaka yetu akitamka; 
" Tunataka dunia ituelewe hivyo". Akaonyesha pia kuwa taifa lina marafiki kwa kutamka;
" Marafiki zetu kwanza tuacheni, tumwonyeshe mshenzi huyu!"
Naam, katika maisha, mwanadamu kuna wakati unalazimika kuingia vitani. Unalazimika kupambana kudai haki yako na kulinda hadhi yako.  Hayo ni mapambano ya haki. Na vita ya kudai haki ni vita ya lazima kupiganwa.
Hapo mwanadamu anakuwa kwenye matatizo. Katika hali hiyo, anachohitaji mwanadamu ni kuungwa mkono na marafiki zake. 
Katika hilo, kama alivyotamka Martini Luther King Jr, kwamba ukimya wa marafiki unaumiza zaidi kuliko kelele za maadui.
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.


Ndugu zangu,

Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.

Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.

Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 

Posted On Friday, 15 February 2013 08:49

6 ef35d

Ndugu zangu,

Kwenye vyombo vya habari juma hili, moja ya habari kubwa iliyochagizwa sana ni kitendo ch viongozi wa Chadema kutoa kwa wananchi, pale viwanja vya Mwembe Yanga, namba za simu ya mkononi ya  Spika Anne  Makinda na Naibu wake, Job Ngugai.

Kimsingi, viongozi wa Chadema waliofanya kitendo kile walikosea. Yawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kuwa Spika na Naibu wake wanaisiginya demokrasia ndani ya Bunge ni madai ya msingi, lakini, namna waliyochagua ya kufikisha madai hayo kwa wananchi haikuwa sahihi.

 

Posted On Friday, 15 February 2013 07:18

.Bonyeza hapa kusoma Mengine

Posted On Friday, 15 February 2013 05:20

 

IMG_0106

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Leveque,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]

IMG_0165

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Cuba  nchini Tanzania Jorge Luis Lopes,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Posted On Friday, 15 February 2013 03:14

8E9U0007

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Askofu Mstaafu Jimbo katoliki la Moshi,Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa ibada ya mazishi Iliyofanyika katika Kanisa la Kristu Mfalme mjni Moshi jana.

PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU

 

Posted On Thursday, 14 February 2013 22:32

1

Mama Salma Kikwete akimpa pole Mama Hawa Ghasia huku akilia kwa uchungu kutokana na msiba wababa yake mzazi   Abdulrahman Ghasia, jana katika Kijiji cha Naumbu, mkoani  Mtwara. (Picha na Bashir Nkoromo)

 

Posted On Thursday, 14 February 2013 22:27

imagesRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya jana, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na waumini wa Dayosisi ya Kaskazini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuuaga mwili wa askofu wa jimbo hilo, Askofu Dkt. Thomas Laizer.

 

Posted On Thursday, 14 February 2013 22:14

 

 

3

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anakata utepe wa lango la kuingia katika ukumbi wa World Garden uliozinduliwa leo jijini Arusha.
1

Ukumbi wa World Garden unavyoonekana kwa mbele.

2

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na wageni waalikwa wakitembelea ukumbi wa disco wa World Garden mara baada ya kuuzindua.

 

Na: Woinde Shizza ,Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa huo katika madhari  na hadhi ya jiji. Aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya

Posted On Thursday, 14 February 2013 14:51

001 e0f1f

 

Ndugu zangu,

Nasoma magazetini, kuwa TFF kumechafuka, kisa? Mbio za Urais; Malinzi na Nyamlani. Mie pia naadika haya nikiwa kama Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF. Naam, bado natembea na kura yangu mfukoni.

Na sisi wanadamu huwa tuna hamu sana ya kuona ' Kinyang'anyiro'. Hivyo, ninaposikia kuwa kwenye Mkutano Mkuu, na kwenye nafasi ya Urais, nitakwenda kuchagua kati ya Nyamlani na Kivuli, basi, ile hamu yangu ya kuona kinyang'anyiro imenitumbukia nyongo...

 

Posted On Thursday, 14 February 2013 11:57

 

GEDSC DIGITAL CAMERAKaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Zuberi Mwombeji na Mkuu wa askari wa hifadhi ya wanyama pori kwa Jamii kutoka Enduimeti Bw. Joseph Laizer wakionyesha madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikamatwa eneo la Mbuga nyeupe lililopo wilaya ya Longido Mkoani Arusha.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Na: Rashid Nchimbi wa jeshi la Polisi Arusha

Mtu mmoja aitwaye Joseph Loiruku Manina Mkazi wa Losinoni wilayani Arumeru anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani hapa baada ya kukutwa na magunia 26 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa kwa kutumia wanyama aina ya Punda toka eneo la Losinoni lililopo wilaya ya Arumeru kwenda nchi jirani ya Kenya ambapo kila Punda alikuwa amebeba magunia mawili. Hayo yameelezwa na

Posted On Thursday, 14 February 2013 10:06

asas1 5be77

Hoyce Temu Alipotembelea Kiwanda Cha Kusindikika Maziwa Cha Asas ' Asas Dairy' kilichopo Iringa. Pichani pia ni Bw. Salim 'Asas' Abri, mfanyabiashara, mdau wa masuala ya kijamii na mkulima maarufu mkoani Iringa.

asas a2f64

Posted On Thursday, 14 February 2013 09:51

dauNa: Gladness Mushi -Arusha

 Mfuko wa hifadhi ya jamii hapa nchini(NSSF)umesema kuwa kwa sasa unaandaa mpango maalumu ambao utalenga kuondokana na Umaskini wa Nchi ya Tanzania huku mpango huo pia ukiongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile Ajira na Vipato vya wananchi.Hayo yameelezwa  Leo mjini Arusha na

Posted On Thursday, 14 February 2013 09:54

 

untitled 05130

Mkutano wa Kumi na Moja wa Baraza la Mawaziri wanaohusika na Masuala ya Bonde la Ziwa Viktoria ulioanza katika Ngazi ya Wataalamu tarehe 10 Februari utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu wakuu tarehe 13 Februari na utakamilishwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 14 Februari 2012. Mkutano huo umefanyika mjini Kisumu Kenya kunzia tarhe 10-14 Februari, 2013.

Posted On Thursday, 14 February 2013 09:22

Swahili Fashion Week Znz 2013 poster 35563

Posted On Thursday, 14 February 2013 08:23

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji