We have 226 guests and no members online

Watumishi

Lema Kufuru

Apokewa kifalme, amkamia Pinda bungeni

na Grace Macha, Arusha

MAPOKEZI ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) yametingisha Jiji la Arusha.

Umati mkubwa wa watu ulijitokeza kwenye mapokezi ya mbunge huyo jana kuanzia njia panda ya kutokea Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo msururu mrefu wa magari, bodaboda na baiskeli ulipamba mapokezi hayo.

Lema aliyekuwa akitokea jijini Dar es Salaam ambapo Mahakama ya Rufaa ilimrejeshea ubunge wake juzi, alikuwa kwenye gari la wazi huku akipungia wananchi.
Kwenye baadhi ya miji ya Wilaya ya Arumeru, alilazimishwa kusimama kutokana na wananchi kumzuia wakitaka awasalimu.

Hali hiyo ilisababisha safari kutoka KIA hadi jijini Arusha ambapo kwa kawaida hutumia saa moja, kuchukua zaidi ya saa sita, kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tisa alasiri kufika jijini Arusha.

Baada ya kufika Arusha, msafara huo ulipita kwenye barabara mbalimbali za jiji hilo, ikiwemo ile ya Afrika ya Mashariki, Goliondoi, Sokoine kisha kuingia kwenye Uwanja wa Kilombero walikofanyia mkutano, ambapo kote walipokuwa wakipita wananchi walikuwa wamejaa barabarani wakimpungia huku wengine wakiwa wamebeba majani kuashiria amani.

Posted On Sunday, 23 December 2012 16:49

Kibamba: Serikali Imeleta Tabaka La Elimu

na Andrew Chale

MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba Nchini, Deus Kibamba, amesema serikali imeweka tabaka katika elimu hali inayochangia kiwango cha elimu katika ngazi ya juu kushuka ikiwemo kushindwa kuvipatia mikopo vyuo vinavyotambulika na mamlaka husika.

Kibamba aliyasema hayo jana kwenye mahafali ya 11 ya chuo cha uandishi wa Habari cha RCT, ambapo alisema kuwa ukubwa wa chuo hicho unatosha kuwapatia hadhi wanafunzi wake kupewa mkopo kwa kuwa kinatambulika na NACTE.

Posted On Sunday, 23 December 2012 16:49

Bibi Achinjwa Kama Kuku

SIKU mbili baada ya mwendesha bodaboda wa mjini Musoma kuchinjwa na kuporwa pikipiki, mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Kwibara wilayani Butiama mkoani Mara, Tabu Makanya (68), ameuawa kwa kukatwa na mapanga kisha kuchinjwa mithili ya kuku na watu wasiojulikana.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika katika kijiji hicho kilichoko Kata ya Mugango baada ya wauaji wanaokadiriwa kufikia wanne, kuvunja mlango wa nyumba aliyokuwa amelala bibi huyo na wajukuu zake wawili.

Habari zinasema kuwa, wauaji awali waliomba kupatiwa simu na fedha na baada ya kukosekana kwa vitu hivyo, waliwaamuru wajukuu wa binti huyo kutulia wakati wanamcharanga kisha kumkata kichwa chake chote.

Mmoja wa watoto wa marehemu, Nyasinde Marubira, aliliambia Tanzania Daima Jumapili nje ya chumba cha kuhifadhia maiti mjini Musoma kuwa, mauaji hayo yamewaumiza na akadai huenda yanatokana na imani za kishirikina.
Alisema baada ya kuamriwa kujifunika kichwa, alisikia watu hao wakisema “leta panga kata kichwa” huku mama yake akipiga kelele na baada ya hapo kukawa kimya.

Posted On Sunday, 23 December 2012 16:49


Tanzania Yaziba Milango Kwa Wanaotaka Kununua Ardhi

 

 

Tanzania sets ceiling for investors to curb land grabbing 

By Correspondent

23rd December 2012 

Tanzania has set a ceiling for investors wanting to buy its agricultural land, a move welcomed by land rights campaigners.

From January 2013, Tanzania will start restricting the size of land that single large-scale foreign and local investors can "lease" for agricultural use. The decision follows both local and international criticism that major investors are grabbing large chunks of land here, often displacing small-scale farmers and local communities.

 

The permanent secretary in the prime minister's office, PenielLyimo, confirmed that the government would limit the amount of land leased to investors in this east African nation. Previously, there were no limits.

Posted On Sunday, 23 December 2012 16:49

 

Makamu Wa Rais Awatembelea Wazee Wa Mkokotoni Kasikazini Unguja

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee, Ali Mohamed Juma (85) Mkazi wa Mkokotoni Shangani Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati alipokuwa katika ziara yae ya kuwatembelea wazee kwa ajili ya kuwajulia hali, leo. Mzee huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu...

Posted On Sunday, 23 December 2012 16:49
Rage Akutana Na Rais Wa Timu Ya Fanja Oman
Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage akiwa na mwenyeji wake Rais wa timu ya Fanja ya Oman...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
A Taste Of ' Village Hall Meeting'- Mahango - Madibira

Leo asubuhi. Nilipata bahati ya kuzungumza mbele ya madiwani wa kata mbili za Madibira na Miyombweni; Waheshimiwa Sanga na Luwekelo. Kulikuwa na watendaji wa kata zote mbili. Kulikuwa na walimu wakuu wa shule nne za za msingi za kata. Kulikuwa na wenyeviti wa kamati za shule. Kulikuwa na wajumbe wa kamati. Jumla ya watu wapatao 15. 
Nilie...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Sihitaji Ulinzi, Ninao Makamanda Wangu!
Wawili mbele, na wawili nyuma. Leo hata kamanda mwenye mafua alijikaza na kujiunga kwenye msafara wa kwenda kijijini Mahango- Madibira....
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22

Magazeti Leo Jumapili

 

Magazeti Leo Jumapili

Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Kipanya Leo...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Tafsiri Yangu Wiki Hii

Tafsiri Yangu Wiki Hii

Tafsiri Yangu Wiki Hii...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Azonto Night...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Mandhari Nzuri Hii......
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22

Ombaomba 14 Kurudishwa Makwao
OMBAOMBA1 4 watasafirishwa makwao baada ya kukamatwa ndani ya Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani na Nje ya nchi , Ubungo (UBT), wakiishi kama makazi yao ya kudumu kinyume cha sheria.
 Akizungumza na Fullshangweblog  jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Kituo hicho Juma Iddi, alisema ombaomba hao walikamatwa wiki moja iliyopita na...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22
Kamanda Olle Ana Mashabiki Wake Madibira....
Kamanda Olle Ana Mashabiki Wake Madibira....

Wasomaji wa uhambuzi wake wa soka kwenye Mwanaspoti. Pichani ni jana alasiri, Madibira.
...
Posted On Sunday, 23 December 2012 12:22

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart