We have 74 guests and no members online

Simu

chamwino c7b7e

Obama's Annex in Dodoma.Orijino iko Chikago.

Posted On Monday, 04 February 2013 14:25

DSC 0653 31561

Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (mbele katikati)akiwasili Zanzibar kwa ziara ya Siku mbili kwa ajili ya kutembelea sehemu za Mji mkongwe na kukutana na Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar, wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, Habari Utamaduni Utalii na Michezo pamoja na Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto,hapo Serena Hotel Zanzibar.
 
                             PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.        

 

Posted On Monday, 04 February 2013 14:19

ECOBANK 4 bbc3f

 

Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi. Wakishiriki katika

Posted On Monday, 04 February 2013 14:10

IMG 8497 55136

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza katika mkutano na waandishi wa vyombo vya habari aliokutana leo katika ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani.

                                                  (PICHA NA TUME YA KATIBA)

 

Posted On Monday, 04 February 2013 14:00

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akimlaki Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyewasili nchini usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. Waliobaki nyuma ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou, Balozi wa

Posted On Monday, 04 February 2013 13:27

 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki(Pichani)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Bwana David Hayes kwa pamoja watazindua Kituo cha Wageni cha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (Wildlife Management Area - WMA) cha Burunge Mkoani Manyara na kukikabidhi kwa wananchi. Uzinduzi huo

Posted On Monday, 04 February 2013 13:16

955863208

                            

Tiketi kwa ajili ya pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon (Indomitable Lions) zinaanza kuuzwa kesho (Febaruari 5 mwaka huu) katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

 Viingilio katika pambano hilo litakalochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni ni sh. 5,000 (viti vya kijani), sh. 7,000 (viti vya bluu), sh. 10,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B na sh. 30,000 VIP A.  Vituo vitakavyouzwa tiketi hizo kuanzia saa 2 asubuhi ni

Posted On Monday, 04 February 2013 13:06

a1 534fb

Kwa mujibu wa Mtafiti, Dr. Brizendine, baadhi ya wanaume wana haraka ya kufanya sex. Kama ni mpira, basi, tungeweza kusema, kuwa baadhi ya wanaume wana haraka ya ' Kufunga magoli'. Utafiti unaonyesha, kuwa mara tu mwanamme anapopata mawasiliano na mwanammke anayempenda, ubongo wake unamwelekeza kwenye fikra za kufanya sex, na atataka afanye haraka. Kwanini?

Ubongo wa mwananme unamfanya awe na ' njaa' ya kutaka zaidi. Kama ni namba ya simu aliyopewa na mwanammke, basi, atataka ampigie siku hiyo hiyo, na ikiwezekana wapange watakutana wapi siku inayofuata kama si siku hiyo hiyo. Kubwa ni kufanya sex. Wanaume wengi waliofanyiwa utafiti, wameonyesha, kuwa kusubiri juma moja au mwezi mmoja kwao ni muda mrefu sana.

Kitendo hicho mara nyingi hakimwongezei mwanamke hamu ya sex, badala yake, kinamtisha na kumfanya awe mwangalifu zaidi.

Na Bi Mkora anasemaje kuhusu hili;

" Yaani, kwa mie mwanamke, mwanamume kama huyo wala simhitaji. Ushauri wangu kwa wanaume ni huu; kama ukiona mwanamke hataki kukimbiia kufanya tendo la ndoa, basi, ujue huyo aweza kukufaa kwa mahusiano ya muda mrefu."- Bi Mkora.

Wengine mnasemaje?

 

Posted On Monday, 04 February 2013 09:01

 

                                   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba 

 

WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa lengo la kufanya uhalifu. Hata hivyo majambazi hao ambao walimfunga kamba mlinzi wa nyumba hiyo na...

Posted On Monday, 04 February 2013 08:45

 

IMG_3368

Kweli kazi ni ngumu lakini yote kwa yote inabidi uifanye na kuifanikisha kwa akili zako zote, na nguvu zako zote ili kukamilisha, na wakati mwingine inabidi kusaidiana kama anavyoonekana katika  Bw. John Bukuku wa Fullshangweblog akimsaidia rafiki yake Mpiganaji mwenzake Adam Gile ili...

Posted On Monday, 04 February 2013 08:10

d2 49a9d

 

Ndugu zangu,

Kama Bob alivyoimba ndivyo nilivyojisikia asubuhi hii hapa Dodoma;

" Rise up this morning, smiled with the rising sun"- Bob Marley

Naam, nimeingia Dodoma jana usiku. Leo asubuhi sana nimeianza siku kwa jogging huku jua likichomoza.

Ndio, hapa Dodoma kuna taarifa kuwa CCM na Chadema jana wametiana kabali. Ni mambo madogo sana kwenye siasa, ingawa hayapendezi. Na kisa haswa? Eti, walikuwa wanagombea mti wa bendera! Ama, Afrika kila kukicha hakukosekani kioja, Plotemy, mwanafalsafa wa Uyunani ya Kale alipata kusema. Na Wahehe wanasema; Isenga imboofu na Isenga indenyefu... kwamba ng'ombe kipofu na aliyevunjika mguu wote ni sawa tu!

Basi, asubuhi hii nimekimbia mchakamchaka wangu kwa kupitia mitaa ya Chamwino. Kuanzia Sokoni Chamwino hadi eneo la Chang'ombe. Njiani nimeona na kusikia mengi. Moja zuri kabisa ni kuyaona mabadiliko kule Chamwino. Kuna maendeleo yamefanyika. Nimeona barabara ya lami mpya iliyojengwa kukatisha Chamwino hadi Chang'ombe. Na miundo mbinu ya mitalo ya maji pia imeboreshwa. Ni tofauti na mara ya mwisho nilipokuwa Dodoma.

Na pale Chan'ombe nilisimama kusikiliza ' Bunge la Wananchi'. Ndio, Chang'ombe pale kuna kijiwe kikubwa cha kahawa. Watu walikuwa wengi, tena asubuhi sana hata kabla ' Waheshimiwa' Wabunge wa Bunge la Muunganohawajaamka kujiandaa na kikao cha Bunge cha leo.

Mada niliyoikuta ilimhusu Benjamin Mkapa. Kiukweli Mkapa anaonekana yuko juu kwa sasa. Watetezi wa Mkapa wanamkumbuka Ben kwa misimamo yake.

" Yule jamaa bwana ( Mkapa) enzi zake akisema jambo analoliamini  analisimamia, hajali kama watu watafurahia au la"- Anadai mtetezi wa Mkapa kwenye Bunge la Wananchi, Chang'ombe , leo asubuhi.

Naam, mengi nimeyasikia katika dakika chache nilizozimama pale kusikiliza.

Taratibu nikaendelea na jogging yangu kurudi nilikofikia. Njiani kwenye kona moja ya Chamwino nikawakuta baadhi ya watu wamesimama nje ya nyumba. Fikra zangu haraka zilinipeleka kuwa kuna jambo limetokea; hapana, kilikuwa kituo cha Daladala!

Fikiri mwenye nyumba unapotoka nyumbani kwako kila asubuhi  unakutana na abiria wa daladala barazani kwako!

Well, " Don't worry, about a thing,

Cause every little thing, is gonna be alright!"- Bob Marley.

Maggid Mjengwa,

Dodoma

0788 111 765

 

 

Posted On Monday, 04 February 2013 06:54

6-waziri-wa-elimu-Shukuru-kawambawa-akionyesha-baadhi-ya-vitabu 08909

Wabunge wa upande wa upinzani wametoka bungeni kama ishara ya kutoridhishwa mfumo wa elimu hapa nyumbani, hoja hiyo binafsi iliwasilishwa na mbunge wa viti maalum Bwana James Mbatia, lakini naibu spika aliipuuza hoja hilo licha ya kwamba ni hoja muhimu sana kwa jamii ya Watanzania.Tatizo la kuzorota kwa elimu hapa nchini halikuanza leo, ni tatizo sugu ambalo limeshindikana kupata

Posted On Monday, 04 February 2013 07:22

3-Mh Balozi Dianna Melrose akisema machache 27d4a

                                          

5-Mh Balozi Dianna Melrose akifanya mahojiano na wanahabari Freddy Macha  na Urban Pulse  1 1664a

 Balozi Dianna Melrose akifanya mahojiano na mwanahabari Fredy Macha,na Urban Pulse

Picha na Urban Pulse

Na: Freddy Macha

Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Dianna Melrose ameeleza furaha yake kuteuliwa kufanya kazi nchini kwetu na kukiri kwamba anauchangamkia wadhifa huo atakaouanza karibuni.Balozi Melrose alikuwa akiongea katika sherehe ya chakula cha jioni iliyofanywa kwa heshima yake nyumbani kwa Balozi wetu wa Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe na mkewe Joyce Kallaghe jijini London Alhamisi iliyopita “Nimebahatika sana.” Alikiri Mama Melrose. “ Watanzania ambao nimekutana nao wana

Posted On Monday, 04 February 2013 06:56

warioba a33f9

Hii ni kuwakumbusha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba atakutana na Wanahabari, leo, Jumatatu, saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Tume, barabara ya Ohio, Dar es Salaam. Katika mkutano huo, atazungumzia tathmini ya mikutano ya Tume na viongozi na Makundi mbalimbali na hatua inayofuata ya utekelezaji wa kazi za Tume. Vyombo vyote vya habari vinakaribishwa.

 

 

Posted On Monday, 04 February 2013 06:43

kp01022013 26e6d

Posted On Monday, 04 February 2013 06:35

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu