We have 60 guests and no members online

Simu

22

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika sherehe hizo.

Posted On Monday, 04 February 2013 06:31

 

Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma 

Na: Ibrahim Bakari, Dodoma na Raymond Kaminyoge, Kigoma 

SHEREHE za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.Vurugu hizo

Posted On Monday, 04 February 2013 06:25

aa1 a7863

Mshambuliaji Said Mohamed Zubeir "gaza"  wa Bandari, jezi ya bluu ( kulia) akikokota mpira.

Picha na Martin Kabemba.

Posted On Monday, 04 February 2013 06:06

IMG-20130204-00692 1f86d

Bonyeza hapa kusoma mengine

Posted On Monday, 04 February 2013 05:33

bara1 55137

Leo nimetoka nacho Iringa saa nane na nusu. Nikasimama Migoli, Mtera na Chipogolo, na bado nimeweza kuingia Dodoma saa moja usiku!

Posted On Sunday, 03 February 2013 21:31

bara dcf1f

Moja ya barabara kongwe barani Afrika. Inapita Iringa. Unapata hisia za kipekee unapoendesha kwenye barabaraba hii. Mimi naamini, kuwa ni barabara kubwa na tulivu kwa sasa katika Tanzania nzima. Unaweza kwenda safari nzima ya kilomita zaidi ya 270 na bado ukaweza kuhsabu ni magari mangapi umekutana nayo. Tanzania yenye amani na utulivu iko kwennye The Great North Road. Njia nzima hukutani na trafiki wala kuona ajali ya barabarani. Ni njia yenye mandhari ya kupendeza sana pia. Pichani ni leo jioni, basi hilo aina ya Leyland Albion nilikutana nalo maeneo ua Chipogolo.

Posted On Sunday, 03 February 2013 21:27

002.BANANA 8a124

Mfanyabaishara wa kuku katika kituo cha daladala eneo la Banana Ugonga jijini Dar es Salaam, Mussa Nangwali akiangalia simu aina ya GT-E 2232 Sumsung yenye line mbili inayouzwa kwa shilingi elfu 80 wakati Vodacom Tanzania walipokuwa wakifanya promosheni ya kuwajuza wananchi pamoja na wateja wake kuwa imeboresha mtandao kwa ajili ya kuwafikia wananchi mahali popote Tanzania,Kulia ni Mwangalizi wa promosheni hiyo Said Akungoni.

Posted On Sunday, 03 February 2013 15:25

 

great dc52f

Great north road hii. From cape to cairo. The road I love to drive through!

Posted On Sunday, 03 February 2013 14:39

wachina f9197


Ndugu zangu,
Jeshi la Wachina linakuja, wako wengi. Kwenye moja ya picha za magazetini hii leo, inamwonyesha Rais wetu akiwa amezungukwa na Wachina.

Rais amevalia ' Kijamaa', lakini Wachina wamevalia ' Kibepari'.

Naam, China ni taifa kubwa kiuchumi. Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa, ni uchumi wa Kibepari.

Posted On Sunday, 03 February 2013 14:23

22

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa  sherehe kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Chama cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani Humo.

23

Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maandamano hayo wakimshangilia Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiongea nao.

 

Posted On Sunday, 03 February 2013 09:58

IMG-20130203-00689 bd1f3

Posted On Sunday, 03 February 2013 09:44

urambo 46aceNdugu zangu,
Wanazuoni wa Kiislamu ni wenye kufahamu zaidi juu ya kisa kifuatacho nilichokipokea miaka mingi iliyopita. Hivyo, wanaweza kukiboresha zaidi.

Inasimuliwa, kuwa katika wakati wake, Mtume Muhammad (S. A. W) alipata kupokea makusanyo ya zakka kutoka kwa mjumbe wake.

Mjumbe yule katika kupita kwake na kukusanya zakka, huko alipewa pia zawadi mbali mbali. Basi, alipofika kwa Mtume na kukabidhi zakka, akaweka kando zile zawadi alizopewa na waja wa Mwenyezi Mungu. Akakabidhi tu kile alichoambiwa akusanye kama zakka.

Posted On Sunday, 03 February 2013 09:34


Moto umewaka katika ghorofa ya 11 ya jengo la PPF.kwa juhudi za zima moto taarifa zinasema kuwa moto umedhibitiwa na sasa hakuna moto tena

Posted On Sunday, 03 February 2013 09:09

a1 dbde2

 

Kwa mujibu wa utafiti wa Daktari Brizendine, tofauti na mwanammke, tangu umri wa kubalehe, ubongo wa mwanamme umeumbwa  ukiwa na nafasi kubwa yenye  kuweza kusajili hofu. Unapeleka nguvu za kushambulia pia, kutumia misuli zaidi. Wenye kumpelekea mwanamme kuwa na hulka za kujilinda na zaidi kulinda eneo lake la miliki, hata kwenye mahusiano. Homoni hizi huchochea nguvu za kushambulia kwa madhumuni ya kujihami.

Ni katika hali hii, ndipo baadhi ya wanaume huwa tayari kufa  kuwapigania wapenzi wao.

Swali ni hili, je, kuna utafiti, ama uzoefu wenye kuonyesha kuwa mwanamke naye kwenye ubongo wake anazo homoni na misuli yenye kumfanya aweze kuwa tayari kufa kumpigania mpenzi wake? Maana, tumeona pia, katika maisha, wanawake waliojitoa muhanga kwa ajili ya wapendwa wao.

Bi Mkora na wengine, tunakaribisha maoni yenu...

Posted On Sunday, 03 February 2013 06:45

3 faf93

Ndugu zangu,

Mpaka kufikia saa moja asubuhi ya leo hakuna hata mmoja aliyeomba lifti yangu ya kwenda Dodoma. Hata wa kushukia Ruaha Mbuyuni, Mikumi na Msamvu hakupatikana! Tena lifti ya buree.

Najiuliza; tatizo ni waomba lifti au mimi mtoa lifti?

Labda masharti yangu yalikuwa magumu. Lakini, sibadili hata sharti moja, na milango ya Kifaru changu bado iko wazi kwa anayetaka lifti ya kwenda Dodoma kutoka Iringa.

Asubuhi Njema!

Maggid,

Iringa.

Posted On Sunday, 03 February 2013 06:38

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi