We have 474 guests and no members online

Watumishi
Unique Model Kuanzia Lamada Hotel
Washiriki wanaowania taji la mwanamitindo mwenye sifa za kipekee Unique model 2012 wanatarajiwa kuanza mazoezi ya miondoko ya kimaonyesho alhamisi hii katika hoteli ya Lamada iliyopo jijini Dar. Jumla ya washiriki kumi na mbili wataanza mazoezi hayo kwa nia ya kujifua kimazoezi ya kutembea miondoko ya kimaonyesho na dansi ili kuukabili mchuano...
Posted On Tuesday, 18 December 2012 04:18
Chipolopolo Kuwasili Kesho

<!--[if gte mso 10]> /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;...
Posted On Tuesday, 18 December 2012 04:59
Cheka Na Chimwemwe Kuumana Ethiopia
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DECEMBER 18, 2012

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.

Mpambano huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika...
Posted On Tuesday, 18 December 2012 05:15
Mwanamke Dereva Wa Basi La Shabiby


 
NUSRA Maguluko (28) ni msichana jasiri na anayependa kujaribu na kupata mafanikio ya majaribio yake bila woga wala kujali ni aina gani ya kazi anayotakiwa kufanya yeye kama mwanamke na ipi asiyostahili kufanya yeye kama mwanamke.
Ni ujasiri wake hasa ndiyo ulimuwezesha kumfikisha hatua aliyonayo kwa
...
Posted On Tuesday, 18 December 2012 05:37

JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa.

Posted On Thursday, 29 November 2012 16:30

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 57. Kituo cha televisheni cha serikali kimetoa taarifa hiyo baada ya kuwepo wiki kadhaa za wasiwasi kuhusiana na afya yake.  Zenawi alilazwa hospitali mwezi uliopita ambapo ugonjwa uliokuwa

Posted On Thursday, 29 November 2012 16:28

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amejitoa kusikiliza rufaa ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, badala yake nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.

Posted On Thursday, 29 November 2012 16:27

Leo hii nimeamua rasmi kurudi CCM, chama ambacho nimekifahamu kwa miaka 35 sasa.

Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha kwenye level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana , Namibia au hata baadhi ya nchi za Ulaya.

Niliamua haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi yatokeayo nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbali mbali.

Nilifanikiwa kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga mikakati ya kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua matawi nchi nzima na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo mmoja. Pia nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.

Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache niliamua kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.

NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA KUJENGWA!

SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.

Posted On Tuesday, 18 December 2012 10:52

Cazorla wa Arsenal angefungiwa mechi tatu
Na Olle Bergdahl Mjengwa,

KATIKA mchezo wa mpira kuna wachezaji wengi wanaopenda kujiangusha bila kuguswa. Wachezaji hawa wanaharibu mchezo wa mpira. Nitawapa mfano uliotokea wiki mbili zilizopita. Arsenal walicheza mechi dhidi ya Westbrom. Katika kipindi cha kwanza Cazorla alipata mpira ndani ya 18 ya Westbrom. Jonas Olsson, beki wa Westbrom alienda kumkaba Cazorla. Olsson alijaribu kupiga mpira, lakini, Cazorla aliupeleka mpira kushoto, Olsson aliukosa mpira na ilionekana kama Olsson aliupiga mguu wa kulia wa Cazorla. Cazorla alianguka na Arsenal walipata penalti.

Marudio yalionyesha kwamba Olsson aliukosa mpira, lakini, pia marudio yalionyesha kwamba Olsson hakugusa mguu wa Cazorla na Cazorla alianguka bila kuguswa.
Inasikitisha kwamba mchezaji mzuri kama Cazorla anajiangusha makusudi ili timu yake ipate penalti. Katika mpira kwa sasa timu inaweza kushinda mechi kwa sababu mchezaji wao anajiangusha ndani ya 18 na refa anaamua ipigwe penalti.

Msimu huu FA kwa kweli wamejaribu kuwapunguza wachezaji wanaojiangusha katika ligi ya Uingereza. Msomaji utakuwa unajua, kwamba wachezaji wengi katika ligi ya Uingereza msimu huu wamepata kadi ya njano kwa sababu wamejiangusha.Mara nyingi katika ligi ya Uingereza marefa wamefanya vizuri kuwapa kadi za njano wachezaji wanaojiangusha. Lakini, mara kwa mara, na hasa katika msimu huu, marefa wamekosea na wametoa kadi ya njano kwa wachezaji ambao kweli wamechezewa faulo na hawakujiangusha. Kwa mfano, Torres alipata kadi njano ya pili katika mechi dhidi ya Manchester United msimu huu. Lakini, marudio yalionyesha kwamba Torres kweli alichezewa faulo na Johny Evans.

Posted On Tuesday, 18 December 2012 10:40

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akivishwa Shada la Mauwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Abeid Karume Zanzibar akitokea Vyetnam kwa ziara ya siku Nne.

Posted On Thursday, 29 November 2012 14:49

Ndugu zangu,

Maishani kuna kushinda na kushindwa. Hata hivyo, ushindi una gharama. Siku zote, mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Mana, ushindi waweza kuwa ghali mno. Ndio, unaweza kupambana ukashinda, lakini, gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako. Yawezekana watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.

Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui.

Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi". Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu! Ndio, kama unapigana vita ya muhimu. Na kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani. Na kama la, basi, tafuta suluhu, au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).

Posted On Thursday, 29 November 2012 14:46

Pichani mtoto Lukeman Carter na mama yake Karrima Carter wakiwa na Kattie Large (kulia) kwenye mazungumzo kuhusiana na kazi za hisani zenye kulenga kuisaidia jam ii ya Watanzania hususan wananchi wa Mahango, Madibira, Mbarali, Mbeya ambako mtoto Lukeman Carter alishiriki kuanzisha wazo la kusaidia kujenga maktaba ya kijamii ya kuwasaidia watoto na watu wazima. Kwa sasa mfuko huo wa hisani umeshakusanya fedha kuweza kujenga visima viwili vya maji kwa watu wa Mahango. Kazi Njema.

Posted On Thursday, 29 November 2012 14:44

MAELFU ya waombolezaji jana walijitokeza kushiriki mazishi ya msanii Hussein Ramadhan maarufu kwa jina la Sharo Milionea, huku mamia wakizirai baada ya kushindwa kujizuia wakati mwili wake unawekwa kaburini.

Mwili wa msanii huyo ulizikwa jana kijijini kwake Lusanga wilayani Muheza saa 7 mchana, katika tukio lililomshirikisha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.

Waombolezaji walianza kumiminika kijijini Lusanga tangu juzi jioni na idadi yao iliongezeka zaidi jana asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.Sala ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma ambaye baadaye aliamuru jeneza hilo kupelekwa makaburini, ambako waombolezaji kadhaa walipoteza fahamu.

Posted On Thursday, 29 November 2012 14:20

Kushoto ni Makamo wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka akibadilishana mawazo na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Dw, Mohamed Abdul-Rahman.

Picha na Sudi Mnete

Posted On Thursday, 29 November 2012 14:18

Mkuu wa mkoa wa singida

 

Kikundi cha nyota njema kikitumbuiza ngoma ya asili ya kabila la Kinyaturu wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia

Na Elisante John;Singida
Novemba 28,2012.

SERIKALI imeyataka mashirika ya kiraia kushirikiana pamoja, ili kupiga vita na hatimaye kutokomeza kabisa vitendo vinavyosababisha ukatili wa kijinsia, hususani wanavyofanyiwa wanawake na watoto wadogo nchini.

Hayo yamebainishwa mjini Singida na mkuu wa mkoa huo, Dk. Parseko Kone, kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake, yaliyoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Peoples, mjini Singida, jana.

Posted On Thursday, 29 November 2012 13:49

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart